Google PlusRSS FeedEmail

UFUNGUZI WA TAWI LA CCM WASHINGTON, DMV.

 

Katika mikakati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kueneza Itikadi yake na Imani yake kwa watanzania walio wengi zaidi,juhudi zinafanyika katika kupanua na kufungua matawi na mashina zaidi ili kuwafikia watanzania wengi zaidi na kujitangaza kwa kuongeza idadi ya wanachama wake. 

Chini ya mkakati uliopitishwa na kikao cha halmashauri kuu ya Taifa (NEC) jambo hili lilipitishwa na kuazimiwa. Na hivi sasa idadi ya matawi imeongezeka maradufu hasa baada ya kuanza ziara za "AHADI NI DENI'' ambapo viongozi wa chama wanazunguka na wale wa serikali katika kukagua na kuhimiza maendeleo na kutafuta suluhu ya pamoja kati ya serikali na wananchi.

Katika harakati hizo, kutakuwa na Ufunguzi wa Tawi jipya la Chama Cha Mapinduzi., Washington, DMV Agosti 25, 2012. Mahali: Oxford Events Center, 9700 Martin Luther King Jr Hwy, Suite A1, Lanham, MD20774. Muda: Saa 10 Jioni.

This entry was posted in

Leave a Reply