Google PlusRSS FeedEmail

DIWANI KATA YA KWADELO AHAMASISHA MAENDELEO KIAINA

 Mkazi wa Kijiji cha Makirinyi, Khadija Mussa, akikabidhi  kiroba cha alizeti kwa diwani wa Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Omary Kariati kuchangia ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho, wakati wa harambee ya kutafuta fedha za ujenzi wa zahanati, uliondeshwa na diwani huyo, jana. Jumla ya magunia 17 yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, na sh. milioni 9.2 vilipatikana, ikiwa ni pamoja na sh. milioni 7 zilizochangwa na  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
 Diwani Omary Kariati akizungumza na wananchi wa Kata yake wakatiwakati wa harambee ya kuchangisha fedha za kufufua mradi wa maji katika kata hiyo. Sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana. Pia gunia 37 za alizeti zenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe zilichangwa kwa ajili hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo.  akihamasisha uchangiaji wa mradi wa maji katika kata hiyo,
 Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati akiendesha trekta wakati akiwasili kwenye hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji katika kata hiyo Kushoto ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo.
 Wakazi wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, wanakabiliwa na uhaba wa maji safi na salama kwa zaidi ya miaka 20 sasa, kutokana na miundombinu iliyozinduliwa mwaka 1973, na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere,  wakati wa uhai wake,  kufa kwa kukosa uangalizi. Pichani Diwani wa
Kata hiyo, Omary Kariati (wapili kulia) na Msaidizi wake  Bakari Ndee wakionyesha tangi la maji lililozinduliwa na Baba wa Taifa ambalo sasa halifanyi kazi
 Trekta 64 za wakulima wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, ambazo wamezipata kwa jitihada za diwani wa kata hiyo, Omary Kariati kutoka Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT, zikiwa zimeegeshwa eneo la mkutano ulioitishwa na diwani huyo, kwa ajili ya harambee ya kuchangisha fedha
kwa ajili ya kufufua mradi wa maji wa kata hiyo, jana. Wakulima hao walifika na trekta hizo na kuwa mstari wa mbele kuchangia mradi huo wa maji.
 Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati, akionyesha mtaro uliochimbwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake mwaka 1973, kwa ajili ya mradi wa maji katika Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, jana. Hata hivyo mradi huo
ambao ulikuwa ukihudumia watu 1,200 wakati huo, umekufa miaka 20 iliyopita na sasa diwani huyo anaunganisha nguvu za pamoja za wananchi na serikali ya CCM kuufufua. Kwadelo sasa ina watu 11,800.

 Wananchi wa Kwadelo wakiwa kwenye mkutano wa harambee ya kuchangishana fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji uliokufa miaka 20 sasa, bada ya kuzinduliwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake mwaka 1973
 Kariati akiwakaribisha nyumbani kwao waandishi wa habari aliofika nao Kwadelo kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo ya kata hiyo.
 Msichana wa Kwadelo mkoani Dodoma akitumia baiskeli kusaka maji
 Trekta la Kilimo Kwanza nyumbani kwa Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Alhaji Omary Kariati
Wazee wa Kata ya Kwadelo, wakipungua mikono kumuaga Diwani wa Kata hiyo, Omary Kariati, alipokuwa anaondoka baada ya kuendesha harambee kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji

This entry was posted in

Leave a Reply