Daudi Msungu akirudisha fomu ya kuomba kugombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti.
Godwin Kunamnbi akirudisha fomu ya kuomba kugombea Umakamu Mweneyekiti na ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kupitia UVCCM.
Innocent Melleck akirudisha fomu ya kuwania kugombea Umakamu Mwenyekiti.
Suleiman Serera akirudisha fomu kuwania Ujumbe wa NEC kupitia UVCCM
Theresia Mtewele akirudisha fomu kwania nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ujumbe wa NEC, Mjumbe wa Bazara la UVCCM
Vailet Elias Sambilwa akirudisha fomu ya kuwania Ujumbe wa NEC kupitia UVCCM
Jamaa akishangaa baada ya kufumaniwa na kamera yetu, wakati akihaha dakika za mwisho kukamilisha fomu zake ndani ya Ofisi ya Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni na Siasa UVCCM, Sophia Duma, Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar es Salaam, leo mida ya saa 10:45. Mwisho wa kupokea ilikuwa saa kumi kamili.
Hata ilipotimu saa kumi jioni, wawania nafasi mbalimbali walikuwa bado wamo katika ofisi hiyo kuhakikisha wanarejesha fomu zao. PICHA KWA HISANI YA UVCCM BLOG