Google PlusRSS FeedEmail
NA PIUS NTIGA
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Tanzania Bara Mzee PHILP MANGULA, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Bara Mzee JOHN MALECELA na kushauriana kuwa Chama kisiendelee kuwafumbia Macho wanachama wanaokiuka taratibu za Chama.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika  Ofisi Ndogo Lumumba yamelenga kuzungumzia umuhimu wa Chama kuendelea kusimamia ipasavyo kanuni za Chama hasa katika kupata viongozi kupitia chaguzi mbalimbali za Chama.
Katika mazungumzo hayo Mzee MANGULA amesisitiza kuwa viongozi wote waliochaguliwa kwa kutoa rushwa siku zao zinahesabika ndani ya Chama kwani Kamati Ndogo iliyoundwa kufuatilia suala hilo itaanza kuwaita kwa ajili ya mahojiano kila mmoja kwa wakati wowote kuanzia sasa.
Mzee MANGULA amesema Kamati hiyo ambayo ipo chini yake tayari imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wanachama wanaowashutumu wagombea kuchaguliwa kwa kutoa rushwa katika chaguzi mbalimbali za Chama zilizofanyika mwaka jana.
Kwa upande wake Mzee MALECELA amempongeza Mzee MANGULA kutokana na kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara huku akimtaka kusimamia pasipo woga kurudisha nidhamu ya Chama kwa kuendelea kuwachukulia hatua kali viongozi waliochaguliwa kwa njia ya kutoa rushwa ndani ya Chama.

MANGULA NA MALECELA, WAFANYA MAZUNGUMZO‏

NA PIUS NTIGA Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Tanzania Bara Mzee PHILP MANGULA, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mweny... [Read More]

TASWIRA MBALIMBALI ZA SHEREHE ZA MIAKA 49 ya MUUNGANO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. [Read More]


Ndege za kivita zikifanya maonesho katika sherehe za Miaka 49 ya Muungano jijini Dar es salaam leo.
Zenye rangi ya njano zinazomwaga rangi za bendera za Taifa ni ndege za mafunzo na zingine za kijivu
ni za kivita.



MAONESHO YA NDEGE ZA KIVITA KWENYE SHEREHE ZA MUUNGANO

Ndege za kivita zikifanya maonesho katika sherehe za Miaka 49 ya Muungano jijini Dar es salaam leo. Zenye rangi ya njano zinazomwaga rangi z... [Read More]

RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA BANGLADESH, SLOVAK, UGIRIKI NA KUWAIT

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bw John haule  kwa Balozi w... [Read More]

 KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akimkaribisha kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Balozi wa Ubelgiji hapa nchini, Koen Adam, Balozi huyo alipomtembelea kwa ajili ya salam, leo asubuhi.
 KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akimtambulisha Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro kwa balozi huyo.
 KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akizungumza na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini, Koen Adam, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, jijini Dar es Salaam, leo, Aprili 25, 2013. Wapoli kulia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akiagana na huyo baada ya mazungumzo yao. Kushoto ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.(Picha zote na Nkoromo Blog

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AKUTANA NA BALOZI WA UBELGIJI HAPA NCHINI, LEO

 KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akimkaribisha kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Balo... [Read More]

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU MBALIMBALI YA KIKRISTO IKULU

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mkutano na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo alipokutana nao  April 23, 201... [Read More]


IMETAYARISHWA NA MWENDA SULIMAN

UHURU:
SERIKALI KUSAMBAZA SEMBE
Kinu cha iringa kutumika
CAG akabidhiwa rungu
VIONGOZI AFRIKA MSITUMIWE
Rais Jakaya Kikwete amewataka viongozi wa Afrika kutokubali kutumiwa na kusababisha migogoro hususan inayotokana na mipaka au ukabila.
POLISI: UPELELEZI KESI YA LWAKATARE UMEKAMILIKA.
(Habari hii imesharipotiwa)
KORTI YABAINI KASORO KESI YA AKINA ZOMBE
(Habari hii imesharipotiwa)
DR SHEIN ATAKA MAFANIKIO ZAIDI CCM
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais Alli M Shein amewataka wanaCCM kuhakikisha chama kinapata mafanikio na kushinda kila ifikapo  kipindi cha uchaguzi mkuu.
MAHAKAMA YATUPA HOJA ZA MAKADA
(habari hii imesharipotiwa)
WAZIRI HAWA AKEMEA MAMEYA, WENYEVITI.
Waziri wan chi, ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Hawa Ghasia amewaonya mameya na wenyeviti wa halmashauri nchini kuacha kujihusisha na shughuli za kandarasi za miradi.
MBUNE AMVAA OFISA USHIRIKA.
Mbunge James Lembeli amemlipua bungeni ofisa ushirika wa wilaya ya kahama, akidai ni kinara wa wizi wa fedha za wakulima wa tumbaku.
GHARAMA ELIMU YA JUU KUWEKEWA MIKAKATI
Serikali itawasilisha bungeni muswada wa sheria ya mfuko wa Elimu ya juu katika kikao kijacho.
Muswada huo unalenga kuweka utaratibu utakaowezesha kubaini vyanzo mbadala vya kugharamia elimu ya juu.
SERIKALI YAJIZATITI UKUSANYAJI MAPATO.
Serikali imesema inaendelea kutafuta njia za kuongeza vyanzo vyake vya mapato.naibu waziri wa fedha Janet Mbene alisema bungeni kuwa mafungu ya bajeti yataongezeka kwa kadri ya upatikanaji fedha.
UWEKEZAJI WA NJE WONGEZEKA
Mitaji ya uwekezaji kutoka nje ya nchi imeongezeka kutoka dola za marekani milioni 520 (shs bilioni nane) mwaka  2005 hadi dola bilioni 11 (shs trillion sita) mwaka 2011
JK AZINDUA UMOJA WA WAFANYABIASHARA
Rais Jakaya Kikwete amezindua umoja wa ushirikiano baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki.
Uzinduzi huo ulifanyika katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hotel ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es salaam.


HABARI LEO:
BEI YA CHAKULA SASA KUPUNGUA
Kampuni 300 zajitokeza kuzalisha kwa wingi
Kitauzwa nchini na ziada soko la kimataifa.
JALADA LA LWAKATARE KWA DPP
(Habari hii imesharipotiwa)
LEMA AIBWAGA TENA CCM KORTINI
Mahakama ya rufaa yakubaliana na kuu
Waliokata rufaa waamriwa kugharamia.
(habari hii imesharipotiwa\)
UKOLONI WACHANGIA MIGOGORO YA MIPAKA AFRIKA
Rais Jakaya kikwete ameshtumu serza za kikoloni akisema zimechangia migogoro ya mipaka katika baadhi ya ardhi za afrika.
BBADHI YA WABUNGE WA CCM WAKATAA KUIUNGA MIKONO BAJETI
(HABARI HII IMESHARIPOTIWA)
RAIS AMTEUA MKURUGENZI MTENDANI WA TIC
Rais Jakaya Kikwete amemteua Julieti kairuki kuwa kurugenzi mtendaki wa kituo cha uwekezaji.
RUSHWA YASHAMIRI SEKTA YA MANUNUZI:
Mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa umma (PPRA) imesema vitendo vya rushwa katika sekta ya manunuzi ndani ya mamlaka mbalimbali zimeendelea kushamiri ka kiasi kukubwa.
USAFIRI WA UBUNGO WAREJEA.
Usafiri wa treni kati ya ubungo na stesheni umerejea tena jana huku abiria wachache wakijitokeza kupanda.
Usafiri huo ulisitishwa mwezi uliopita.
WANAFUNZI 3900 VYUO WAKOSA MIKOPO
(HABARI HII IMESHARIPOTIWA)
WIZARA YA KILIMO YAKAMILISHA ANDIKO LA VIJANA KUJIAJIRI.
Wizara ya kilimo, chakula na ushirika imekamilisha andiko la namna ya kuwavutia vijana kujiajirti katika kilimo na biashara.

TANZANIA DAIMA:
WATESAJI WA KIBANDA, ULIMBOKA KITENDAWILI
polisi wakosa majibu wadai uchunguzi unaendelea
lwakatere, Ludovick jalada lao lakabidhiwa kwa DPP.
Watesaji wa mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari nchini, DR Ulimboka na mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Kibanda bado kindawili baada ya polisi kudai inaendelea na uchunguzi
NJAA YATIKISA NUSU YA NCHI.
Halmashauri 70 kati ya 136 nchini, zinakabiliwa na janga la njaa kutokana na ukame uliosababisha uzalishaji kuwa mdogo.
LEMA AILIZA TENA CCM
(habari hii imesharipotiwa)
WANA-CUF 11 WAWANIA JIMBO LA CHAMBANI
Wanachama 11 wa CUF wamejitokeza kuwania ubunge katika jimbo la chambani lililo kisiwani Pemba, kutokana na kifo cha mbunge wake Salim Hemed Khamis.
DOSARI ZA HATI ZAKWAMISHA RUFAA YA ZOMBE.
Mahakama ya Rufaa nchini, jana ilishindwa kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na mkurugenzi wa mashitaka (DPP) Dk Eliezer Feleshi.
WABUNGE WAMBANA WAZIRI WA KILIMO
(Habari hii imesharipotiwa)
USHIRIKINA WAZUA BALAA KWA PINDA
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya mizengo Pinda, kata ya kibaoni wilayani Mlele wamemshambilia kwa mawe na matofali mkuu wa shule hiyo na mwalimu wa taaluma  kisha kuharibu jengo la utawala na nyumba za walimu, wakiwatuhumu kujihusisha na vitendo vya uchawi.
WIZARA IPITIE SERA YA UENDESHAJI VYUO BINAFSI.
Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufungi staid imetakiwa kupitia upya sera ya uendeshaji wa vyuo binafsi vinavyotoa mafunzo ya ualimu nchini ili kuviwezesha vyuo hivyo kutoa taaluma yenye tija.
WANANCHI WATAKIWA KUTOTISHWA NA WANAHARAKATI
Wananchi wanaoishi maeneo yaliyogunduliwa na kuwepo na madini ya uranium wametakiwa kutotishwa na maneno ya wanaharakati, kwani serikali haitayarutubisha madini hayo bali kuyachimba na kuyauza nje kama malighafi ili kuepuka madhara..
MAKALA_TENDWA ANALEA UCHOCHEZI WA CCM
Makala inataja matukio mbalimbali ya vyama vya upinzani kuhusishwa na udini na ukabila na kusababisha chuki miongoni mwa watu na kumtaka panda kuikemea CCM kuacha kueneza propaganda hizo chafu.
MNYIKA  ASUBIRI MKUTANO WA RAIS.
Ikulu imetakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu mkutano uliokuwa ufanyike kati ya Rais Jakaya Kikwete na mbunge wa Ubungo John Mnyika.

MTANZANIA:
WABUNGE CCM WACHACHAMAA
Wajimbanga kukwamisha bajeti ya kilimo, Maige, lembele waongoza mashambulizi.
(habari hii imesharipotiwa)
POLISI: KESI YA LWAKATARE IMEIVA.
Jeshi la polisi nchini limetoa taarifa ya kukamilika kwa uchunguzi dhidi ya tuhuma za kuhusika na vitendo vya kigaidi zinazowakabili mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Chadema.
HOMA UCHAGUZI ,ADIWANI ARUSHA YAPANDA.
Mnyukano mkali wa kisiasa, unatarajiwa kuibuka tena juni mwaka huu kati ya CCM na CHADEMA,
TUME YA TAIFA YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO CHAMBANI
(habari hii imesharipotiwa)
RUFANI DHIDI YA ZOMBE YAKWAMA.
(habari hii imesharipotiwa)
LEMA AWABWAGA TENA MAKADA WA CCM
(habari hii imesharipotiwa)
BENKI YA DUNIA YAOKOA BAJETI YA TANZANIA.
Tanzania imepokea mabilioni ya fedha kutoka benki ya dunia WB kwa ajili ya kusaidia bajeti ya 2013-2014 katika miradi ya umeme na gesi.
DC LUSHOTO AWAASA WAISLAMU
Mkuu wa wilaya ya lushoto, Alhaj Majid Mwanga amewataka viongozi wa dini ya kiislamu kuwaelimisha waumini wao kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.
JUKWAA LA KATIBA LAWAPASHA WABUNGE.
M/kiti wa jukwaa la katiba Tanzania (JUKATA) Deus Kibamba amewapasha wabunge kwa kuwaambia kuwa wanapokuwa wakichangia mijadala bungeni wanajali zaidi maslahi ya vyama badala ya wananchi.
MNYIKA HAJARIDHIKA NA MAJIBU YA WASSIRA
Mbunge wa ubungo, John Mnyika (CHADEMA) amesema ofisi yake haijaridhika na majibu yaliyotolewa bungeni na waziri wan chi ofisi ya Rais (uhusiano na Uratibu) steven wassira kuhusu ahadya Rais Kikwete kukutana na mamlaka zinazosimamia huduma ya maji katika jiji la Dar es salaam.
SALMA KIKWETE AWAPA SOMO WANAUME
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wanaume kujenga tabia ya kuongozan ana wake zao wanapokwenda hospitalini kujiunga na uzazi wa mpango.
KINANA ATAFUTA SULUHU YA WAKULIMA, KIWANDA CHA MTIBWA
Katibu mkuu wa CCM ndugu A kinana amefanya mkutano wa pamoja kati ya wakulima na uongozi wa kiwanda cha mtibwa ili kutafuta suluhu ya mgogoro wao unaoendelea.



MWANANCHI:
LEMA KIDEDEA TENA
Dar es salaam; mbunge wa arusha mjini (chadema) Godbless Lema ameibuka kidedea baada ya mahakama ya rufani kutupilia mbali maombi ya marejeo ya rufaa iliyomrejesha bungeni. Maombi hayo yaliwaslishwa na makada watatu wa CCM mkoani Arusha ambao walitaka mahakama ifanye marejeo ya hukumu yake ya awali.
CHC WAKAIDI RIPOTI YA CAG
Dar es salaam: bodi ya shirika hodhi la mali za serikali (CHC)  imelikaidi bunge na kuendelea na utaratibu wa uuzaji wa kiwanja namba 10 kilichopo barabara ya nyerere, Dar es salaam.
BAJETI YA KILIMO: MAIGE, LEMBELI WAIBANA SERIKALI.
Dodoma: wakati Tanzania imetajwa kuwa nchi ya pili kwa umasikini kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, wabunge wameishukia serikali kwa kutenga fedha kidogo kwenye bajeti ya kilimo.
KIKWETE: AFRIKA TUMEPIGA HATUA, TUNAWEZA KUJISIMAMIA.
Rais Jakaya Kikwete, amesema Bara la Afrika limepitia kwenye kipindi kigumu cha kukabiliana na utawala wa kikoloni ulioendesha mambo kwa kuzikandamiza nchi za kiafrika, lakini sasa bara hilo limepiga hatua na linaweza kuzitafutia ufumbuzi changamoto za kiusalama pasipo kutegemea msaada wa nje.
WABUNGE CHADEMA WAAHIDI KUSHAMBULIA KWA MIKUTANO
Dar es salaam: wabunge sita wa chadema waliosimamishwa siku tano kuhudhuria vikao vya bunge, leo wameanza kushambulia kwa mikutano yao katika jimbo la Iringa mjini baada ya kumaliza mwanza.
UPELELEZI KESI YA LWAKATARE UMEKAMILIKA-MKURUGENZI
Dar es salaam: Kaimu Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini, Issaya Mulungu, amesema upelelezi kuhusu tuhuma za vitendo vya ugaidi zinazomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfred Lwakatare na mwenzake umekamilika.
RUFAA DHIDI YA ZOMBE NJIAPANDA
Dar es salaam: rufaa dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es salaam Abdalah Zombe na wenzake wanane, iko katika njiapanda baada ya Mahakama ya Rufani kuibua dosari za kisheria.
SERIKALI YAFUNGA VIWANDA VYA NONDO.
Ni baada ya kuthibitika kuwa nondo zinazozalishwa na viwanda hivyo hazina ubora unaokamilika.
UHURU WA HABARI KUADHIMISHWA.
Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa afrika tawi la Tanzannia litashirikiana na wadau mbalimbaliwa habari nchini kuandaa sherehe ya kuadhimisha miaka 20 ya siku ya uhuru
VICKY KAMATA AWAASA VIJANA KUHUBIRI AMANI
Geita|: mbunge wa viti maalum Geita,Vicky Kamata amewataka vijana kutumia nafasi zao kuliombea amani Taifa, kwani kuna baadhi ya watu wanataka kutumia umaarufu kuivuruga amani iliyopo.
MIKUTANO YA CHADEMA KUENDELEA IRINGA.
Iringa: CHADEMA leo kinatarajia kufanya mkutano wa hadhara uwanja wa mwembetogwa mjini hapa ukiwa ni mwendelezo wa mpango wao waliodai watawashitaki kiti cha spika kwa wananchi.  
BENKI YA DUNIA KUSAMBAZA UMEME BIHARAMULO VIJIJINI
Biharamulo: Benki ya dunia kwa kushirikiana na wakala wa umeme vijijini (REA) zinatarajiwa kusambazwa umeme kwa shule za sekondari sita.
3,800 WAKOSA MIKOPO KUSOMA ELIMU YA JUU
Jumla ya wanafunzi 3821 waliokuwa na sifa ya kwenda vyuo vikuu na kupata mikopo hawajapewa mikopo hiyo.
WAPINZANI WATAKA KUJUA MAFANIKIO YA KILIMO KWANZA
Kambi ya upinzanib imeitaka serikali kueleza kwa kina utekelezaji wa nguzo kumi za kilimo kwanza.

HABARI ZA MAGAZETINI LEO JUMANNE TAREHE 23TH APRIL 2013.

IMETAYARISHWA NA MWENDA SULIMAN UHURU: SERIKALI KUSAMBAZA SEMBE Kinu cha iringa kutumika CAG akabidhiwa rungu VIONGOZI AFRIKA MSITUMIWE Ra... [Read More]


  President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete welcomes former Mozambican President and SADC mediator for Madagascar, Joachim Chissano at Dar es Salaam Serena Hotel during the opening ceremony for the 368th Ministerial Meeting of the Peace and Security Council of the African Union. Looking on isMinister for Foreign Affairs and International Cooperation of the United Republic of Tanzania, Mr Bernard Membe
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his speech during the opening ceremony for the Ministerial Meeting of the Peace and Security of the African Union held in Dar es Salaam this morning.
 A cross section of the delegates and dignitaries who attended the opening ceremony for the Ministerial Meeting of the Peace and Security of the African Union held in Dar es Salaam this morning.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete(Centre) in a group picture with some delegates who attended the opening ceremony of the Ministerial Meeting of the Peace and Security of the African Union held in Dar es Salaam this morning.(photo by Freddy Maro.ternational Cooperation of the United Republic of Tanzania, Mr Bernard Membe

PRESIDENT DR. JAKAYA KIKWETE OPENS AU MINISTERIAL FOR PEACE AND SECURITY IN DAR ES SALAAM

  President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete welcomes former Mozambican President and SADC mediator for Madagascar, Joachim Chissano at Dar es Sala... [Read More]

Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na wakazi wa kata ya Kirongo wakati wa ufunguzi wa kisima cha maji Mkoani Morogoro.



Moja ya Visima Kumi vilivyokamilika ambavyo vipo kwenye mradi wa visima 23 vinavyojengwa kwa gharama  shilingi milioni mia tatu na sitini elfu.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa kisima cha maji kata ya Kirongo,mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Andulrahman Kinana  akimtwisha ndoo ya maji mwana mama wa kata ya Kirongo,baada ya ufunguzi wa kisima cha maji.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wazee wa shina no.2,kata ya Mwembesongo.


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya muwa shina no.2,kata ya Mwembesongo.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na nyuso ya furaha baada ya kupokelewa vizuri na wananchi wa kata ya Mwembesongo,Morogoro. 

Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Andulrahman Kinana akihutubia wananchi wa shina no. 2 kata ya Mwembesongo, ambapo pamoja na kufungua shina hilo la umoja wa wazazi pia alifanya harambee iliyofikia kiasi cha shilingi milioni mbili ,ambazo zitatuika kama mtaji wa shina hilo linalojishughulisha na shughuli za ujasiriamali wa kutengeneza sabuni na mamashughuli za mama lishe.



Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakiwasili kwenye mkutano wa hadhara ,kwenye viwanja vya Shule ya msingi Kiwanja cha Ndege,Morogoro.

Msanii Linah akitumbuiza wananchi wa Morogoro waliokuja kwenye mkutano wa CCM.

Wasanii wa Wanaume Family wakitumbuiza wananchi wa mkoa wa Morogoro wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM.

Msanii Diamond akitumbuiza wakazi wa mkoa wa Morogoro wakati wa mkutano wa CCM katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege,Morogoro.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi akihutubia mamia ya wakazi wa Morogoro kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya msingi Kiwanja cha Ndege.

Robert F. Selasela Diwani wa Kata ya Kiloka akisalimia wananchi waliokuja kwenye mkutano wa CCM, Robet ni mmoja wa Viongozi vijana  walio ndani ya CCM.


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati mkubwa uliokusanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja Cha Ndege,Morogoro.


MATUKIO MBALI MBALI YA HITIMISHO YA ZIARA YA KINANA MKOA WA MOROGORO

Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na wakazi wa kata ya Kirongo wakati wa ufunguzi wa kisima cha maji Mkoani Morogoro. Moja ya Visima Kumi vili... [Read More]

*Asema viongozi wake wamekubuhu wa ubinafsi
*Wanajali maslahi binafsi ya Chama chao badala ya Watanzania
*Awatakja Watanzania kuwapuuza
Kinana akihutubia mjini Morogoro leo.Picha: Bashir Nkoromo
NA BASHIR NKOROMO, MOROGORO
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameisasambua Chadema na kusema ni chama ambacho daima kimekuwa kikiweka mbele maslahi yake binafsi kuliko ya Watanzania.

Amesema viongozi wa chama hicho wamekubuhu kwa udikteta kiasi cha kujiona wao ndio wanajua kila jambo kuliko watu wengine hata mwenzao wa chama cha upinzani ikitokea ana mawazo  au msimamo wasioutaka au ameipongeza serikali kwao huonekana ni msaliti na kibaraka wa CCM.

Akihutubia leo mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika jana mjini hapa,Kinana, alisema kuwa Chadema ni balaa kwa nchi naa watu kwani viongozi wake wamekuwa ni watu wa kuhubiri machafuko badala ya mshikamano uliozoeleka Tanzania.

Alisema kutokana na umangimeza wao sasa Chadema kimeanza kuigawa nchi kwa kutumia sera ya ukanda licha ya kwamba sera hiyoi ni kinyume cha katiba ya nchi na watu wake.

"Ninapenda leo niwaelezeni ndugu Watanzania Chadema ilivyojawa na ubinafsi, wamekuwa wakiwakukusanya Watanzania na kuwagawa kwa sera yao ya majimbo. hili si mara ya kwanza maana katika kipindi cha siku za hivi karubuni walitangaza wazi kuigawa nchi kwa kutaka
kujitenga kanda ya Kaskazini eti ili iwe chini ya utawala wao", alisema Kinana.

Kinana alisema CCM kama chama kilichoingia mkataba na Watanzania haiwezi katu kukaa kimya na kuona hali hii ikitokea, kila mara tumekuwa tukihubiri amani na mshakamano lakini Chadema hili limewashinda jambo ambalo alisema ni dalili kwamba viongozi wa Chadema wameingia katika siasa kwa malengo yao binafsi.

"CCM itaendelea kusema ukweli kwa kila jambo na wala haitaficha hata likiwa siyo la kufurahisha wanachama wake ili mradi ni la kweli, tofauti na  hawa Chadema, lazima Watanzania muwe makini nao kutokana na aina ya siasa na matendo yao wanayojinasibvu nayo" alisema Kinana.

Vurugu za Chadema
Kinana alisema kuwa Chadema wamekuwa ni watu wa maajabu na vurugu kubwa nchini, na katika hilo alitoa mfano ya mambo ambayo wanayafanya bungeni.

"Chadema kazi yao ni vurugu tu, utadhani wao ndio wamekuwa kambi ya upinzani wa kwanza bungeni katika nchi  hii. Walikuwepo wapinzani  kabla yao lakini kama CUF na Kina Mrema (Augustine Mrema) enzi za NCCR Mageuzi lakini hamkupara kushuhudia vituko kama

hawa Chadema ambao wanajiona wao ndio kila kitu. Wanatoa vitisho kila siku kwa Serikali hata kumtukana mkuu wa Nchi bila kujali kwamba ni kiongozi ambaye amefika pele kwa kuchaguliwa na idadi kubwa ya Watanzania", alisema.

"Wanabeza wapinzani wengine , wakiona mpinzani anapongeza kazi iliyofanywa na CCM wanaanza kumshambulia.Hakuna anayejua zadi ya Chadema .Wanamtukana Rais, wanaushambulia usalama wa Taifa, wanashambulia vyombo vya usalama,"alisema Kinana

"Hawa jamaa ni watu wa ajabu sana, kila kitu wanajua wao wengine hawajui.Wakigombana katika chama chao utasikia kuna mkono wa CCM. Sijui ni watu wa aina gani , wanafanya mambo ya ajabu sana kiasi cha kushangaza,"alisema.

Kinana alitoa ushauri kwa Chadema kuwa na uwezo wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao kuliko kutumia muda wao mwingi kila jambo ambalo linakwenda kombo kunyoosha vidole kwa CCM.

"CCM tuna changamoto zetu nyingi, lakini tunatatua matatizo yetu wenyewe hatupotayari.Tuna makundi ndani ya chama lakini hayo ndio mambo ya siasa,"alisisitiza.

Mchakato wa Katiba mpya
Kinana alisema pamoja na kazi nzuri ambayo imefanywa katika mchakato wa Katiba mpya, kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ametoa hotuba yake ambayo inaonesha wazi hakuna ambacho kimefanyika katika mchakato huo.

Alisema kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe akiwa bunge ametumia muda wake mwingi kuzungumzia mchakato wa katiba mpya na kubwa katika hotuba yake kuwa haufai.

"Simsingizii kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni, ndani ya hotuba yake ameeleza wazi kuwa waliopewa dhamana ya kukusanya maoni ya Katiba mpya hawana ujuzi.Hii si kweli, waliopewa dhamana hiyo ni watu ambao wanaifanya kazi hiyo kwa uadilifu,"alisema.

Alisema Chadema ni watu binafsi ambao wao wametawaliwa na uroho mkubwa na wao kazi ni kuangalia maslahi zaidi na ni si maslahi ya nchi.

Ziara yake Morogoro
Kinana alisema kuwa ziara yake amejifunza mamb mengi lakini kubwa na msingi ambalo lipo kwa chama hicho kitahakikisha kinatafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi na hasa migogoro ya ardhi, mipaka na huduma za jamii ambazo nazo ni changamoto kubwa kwa maeneo mbalimbali.

"Ziara yangu na viongozi wengine wa chama chetu ambayo tuimefanya katika wilaya zote za Morogoro tumeona changamoto nyingi.Tumetafuta ufumbuzi wa matatizo lakini mengine yanapatiwa ufumbuzi baada ya kukaa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama na kisha kutoa maagizo kwa Serikali kutekeleza,"alisema.

Agizo kwa wabunge CCM
Katibu Mkuu huyo wa CCM, alitumia nafasi hiyo kwa kuwataka wabunge wa CCM kutembea kifua mbele kwani chama chao kinafanya kazi kubwa lakini aliwataka wawe makini na Chadema na kuwataka kutowasikiliza kwani sasa imetosha.

Alisema Chadema wamekuwa wakisikiliza muda mrefu ndani ya Bunge na kuna wakati wabunge wa CCM walichukia baada ya Rais Jakaya Kikwete kukubali kukutana nao kujadili mchakato wa Katiba Mpya.

KINANA AICHAMBUA CHADEMA

*Asema viongozi wake wamekubuhu wa ubinafsi *Wanajali maslahi binafsi ya Chama chao badala ya Watanzania *Awatakja Watanzania kuwapuuza Kina... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa CCM uliofanyika jioni hii mjini Morogoro jioni hii, ikiwa ni hitimisho la ziara yake ya siku nane mkoani Morogoro.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa CCM uliofanyika jioni hii mjini Morogoro, ikiwa ni hitimisho la ziara yake ya siku nane mkoani Morogoro.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  wakiingia kwenye Uwanja wa mkutano wa hadhara wa CCM mjini Morogoro.
 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano huo
 Maelfu wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa CCM uliofanyika mkoani Morogoro jioni hii
 Msanii Nasibu Abdul 'Diamond' akibebwa na wasanii wake kukoleza, alipotumbuiza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mjini Morogoro leo jioni
 Diamond akitumbuiza kwenye mkutano wa CCM uliofanyika jioni hii mjini Morogoro
 Msanii Lina akitumbuiza kwenye mkutano huo
 Wasanii Chege na Temba kutoka TMK Family wakishambulia jukwaa wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye mjini Morogoro jioni hii
Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Sixtus Mapunda akizungumza mwanzoni mwa mkutano huo

CCM YAFUNIKA MKUTANO WA HADHARA MOROGORO JIONI HII

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa CCM uliofanyika jioni hii mjini Morogoro jion... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM wilaya ya Morogoro mjini, asubuhi hii katika ukumbi wa VETA mkoani Morogoro. Wengine kulia ni Mbunge wa Morogoro mjini Mohammed Aziz Abood, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa CCM wilaya ya Moro mjini  Fukiri Juma na kulia (kushoto wa pili) Innocent Karogelesi
Wajumbe wa nyumba kumi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, alipozungumza nao asubuhi hii kwenye ukumbi wa VETA mjini Morogoro.

KINANA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI MORO MJINI ASUBUHI HII, KUFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA JIONI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM wilaya ya Morogoro mjini, asubuhi hii katika ukumbi wa ... [Read More]

KINANA KUHUTUBIA WANANCHI WA MOROGORO

Katibu Mkuu wa CCM Taifa leo atahutubia wakazi wa Morogoro mjini katika viwanja vya shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege. Katibu Mkuu ambaye an... [Read More]

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya shamba darasa ambapo wanakijiji wanapewa mafunzo ya kufuga na kulima kwa kisasa.

Moja ya banda la Mifugo kwa ajili ya mafunzo ya ufugaji

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma baadhi ya kero za wananchi wa kata ya Kiroka,Morogoro vijijini.

Ujenzi wa Kituo cha afya cha Mkuyuni ukiwa unaendelea kwa kasi nzuri.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana akishiriki ujenzi wa kituo cha afya cha Mkuyuni.

Zahanati ya Mkuyuni ambapo kuna jengwa kituo cha Afya cha Mkuyuni.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa Mkuyuni.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Kijiji cha Mkuyuni,ambapo ujenzi wa Soko jipya na kituo cha Afya vinaenda sambamba,ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Chifu Kingaru,wakati wa kupokea  zawadi za kimila kutoka kwa Chifu huyo wa 14 katika kijiji cha Mkuyuni.

Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa shukrani zake kwa Chifu Kingaru wa 14.

Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza wananchi wa Morogoro Vijijini  kwenda kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na kijana wa Kimasai kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Mvuha,Morogoro Vijijini.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Mvuha ,Morogoro  Vijijini, tarehe 20 April 2013.

KINANA AFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI MOROGORO VIJIJINI

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya shamba darasa ambapo wanakijiji wanapewa mafunzo ya kufuga na kulima kwa kisa... [Read More]