KINANA |
GAIRO, MOROGORO, Tanzania
Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo kinatarajiwa 'kuuteka' mji wa Gairo kitakapofanya mkutano mkubwa wa hadhara kuanzia saa kumi jioni katika mji huo.
Kulingana na shamrashamra na simulizi zilizvyotanda miongoni mwa wananchi katika maeneo mbalimbali hapa Gairo, mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya watu, kwa ajili ya kumshudia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye anakuwa Gairo kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake kushika wadhafa huo.
Mbali na Kinana ambaye aliwasili jana jioni, akitokea Kilosa, viongozi wengine wanaotarajiwa kuwasha moto kwenye mkutano huo,ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Dk. Mohammed Seif Khatib.
Kabla ya mkutano huo Kinana na ujumbe wake wamepangiwa kufanya shughuli mbalimbali za ujenzi wa Chama na ukaguzi wa ilani ya CCM, ikiwa ni pamoja na Kinana kufanya kikao cha ndani na mabalozi na viongozi wa Chama ngazi wa kata zioizopo karibu na makao makuu ya wiyala.
Kaim Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda amesema asubuhi hii kiwamba, baada ya mkutano wa ndani, Kinana atafanya shughuli ya kukagua uhai wa chama katika mashina na matawi katika maeneo mbalimbali wilayani hapa. Imetayarishwa na Nkoromo Blog