Google PlusRSS FeedEmail

KINANA AONGOZA KIKAO CHA WAKULIMA WA MIWA NA WAMILIKI WA KIWANDA CHA MTIBWA

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana (wa tatu toka  kulia) akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Ndugu Innocent  Kalogeris, Katibu wa NEC Itikadozi na Uenezi,Nape Nnauye na viongozi wengine wa wilaya ya Mvomero wakiwa kwenye mkutano wa pamoja kati wa wakulima na wamiliki wa kwanda cha sukari Mtibwa.

Wakulima wa wilaya ya Mvomero pamoja na viongozi wa  kiwanda cha sukari Mtibwa wakiwa kwenye mkutano na  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana 

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro,Ndugu Innocent Kalogeres akifafanua jambo wakati wa mkutano na wakulima pamoja na wamiliki wa kiwanda cha Mtibwa.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwasalimu  Wakulima wa wilaya ya Mvomero wakati wa mkutano kati ya wakuli na wamiliki wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa pamoja na Katibu Mkuu  wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana.

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakulima wa Mvomero na wamiliki wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa ambapo matatizo na kero za muda mrefu kati ya wakulima,wamiliki wa kiwanda cha sukari  cha Mtibwa na wafugaji.

Mwenyekiti wa chama cha wakulima  (MOA) Hadija Kondo akielezea matatizo yanayowakabili wakulima wa Mvomero.


Msemaji wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa,ndugu Hamad Yahya Juma akifafanua masula mbali mbali ambayo yanaleta migogoro kati ya wakulima na kiwanda hicho mbele ya katib.u mkuu wa CCm,ndugu Abdulrahman Kinana

John Mwalisu,Zonal meneja wa PPF akifafanua maswala ambayo wakulima wanalalamika .

Jonnas Van Zeland ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mvomero akizungumzia kwa kina  ubadhilifu mkubwa wa fedha uliofanywa kwenye halmashauri hiyo.

This entry was posted in

Leave a Reply