Google PlusRSS FeedEmail

SADIFAH ACHANGIA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI VYA VIJANA

OMAR SULEYMAN, Katibu wa Uchumi na Fedha wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, akitoa maelekezo kwa vijana wa vikundi vya ujasiriamali vya jimbo la donge juu ya namna ya kutumia fursa ya uwezeshaji iliyopatikana katika kuongeza juhudi na kujituma katika uzalishaji.

Mwenyekiti wa Jimbo la Donge, Ally Maabad akiwa katika mkutano huo ambao Mbunge wa jimbo la Donge Mhe. Sadifah Juma alichangia vikundi mbalimbali vya ujasirimali.

Katibu wa hamasa na Chipukizi Taifa na MNEC Ndugu Omar Justuce akizungumza katika mkutano wa kuchangia vikundi 12 vya vijana wajasiriamali wa jimbo la donge.

Mke wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya  Umoja wa Vijana wa Chama Cha mapinduzi (UVCCM) akiwa anazungumza katika Mkutano wa kuchangia vijana wajasiriamali wa Jimbo la Donge.

Akina Mama waliojitokeza katika Mkutano wa Jimbo la Donge, ambapo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mbunge wa Jimbo hilo Sadifah Juma alikabidhi michango ya fedha taslimu na vifaa vyenye jumla ya kiasi cha shilingi milioni nne.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Taifa, Ndugu Martine Shigela akiwa anazungumza na kusisitiza jambo katika mkutano huo ambapo alisema kuwa wananchi wa Jimbo la Donge wanayo bahati ya kuwa na mbunge anayewajali na kusaidiana nao katika kulijenga na kuliletea maendeleo jimbo la Donge.

Mbunge wa Jimbo la Donge  Mhe. Sadifah akikabidhi mchango kwa moja ya kikundi cha wajasiriamali wanaofanya shughuli za ufugaji wa kuku.

Katibu wa Kikundi cha Ujasiriamali cha mkorofi si mwenzetu akipokea mchango wa shilingi 300,000 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM ndugu Sadifah Juma.

This entry was posted in

Leave a Reply