NA MWANDISHI MAALUM, NEW YORK
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja Azimio linalopendekeza kuidhinishwa kwa hatua zote za Ujenzi wa Mradi wa Taasisi mpya ya Kimataifa itakayochukua majukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR).
Mradi huo wa majengo ya kisasa, utajengwa katika eneo la LakiLaki Jijini Arusha-Tanzania na utahusisha Ofisi, vyumba vya mahakama, na sehemu ya kutunzia nyaraka na kumbukumbu zote za ICTR. Eneo hilo la Laki Laki limetolewa na Serikali ya Tanzania kwa Umoja wa Mataifa.
Baraza Kuu limepitisha Azimio hilo katika mkutano wake uliofanyika siku ya Ijumaa ( April 12),mkutano ambao pia, Baraza lilipokea na kupitisha maazimio mengine Nane yaliyowasilishwa na Kamati ya Tano inayohusika na masuala ya Utawala na Bajeti katika Umoja wa Mataifa.
Taasisi hiyo mpya ijukulikanayo kama Mfumo wa Kimataifa wa Kumalizia Mashauri Masalia ya iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari au kwa kimombo ( International Residual Mechanism for Criminal Tribunal )- Tawi la Arusha pamoja na kuhifadhi nyaraka itasimamia kesi za Masalia ambazo zitakuwa bado hazijakamilia baada ya ICTR kumaliza muda wake mwakani.
Azimio hilo pamoja na mambo mengine, linamtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuweka bayana uwajibikaji na uangalizi wa kina katika ujenzi wa mradi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba, sheria, taratibu, kanuni na miongozo yote ya Umoja wa Mataifa inayohusu manunuzi/ugavi inafuatwa ipasavyo katika utekelezaji wa mradi huu.
Gharama za mradi zinatarajiwa kuwa kiasi cha dola za kimarekani 8.78 Milioni ( takribani Sh.14 Bilioni). Fedha hizi zinalipwa na Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Mradi unatarajiwa kukamilika kabla ya mwishoni mwa mwaka 2015.
Aidha kupitia Azimio hilo, Baraza Kuu pia limeishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea na jukumu la kufuatilia kwa karibu mchakato wote unaohusiana na utekelezaji wa mradi na vilevile katika kuhakikisha kwamba inashirikiana na Umoja wa Mataifa kufanikisha Mradi huu.
Halikadharika kupitia Azimio hilo, Baraza Kuu limeelezea kufurahishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi hasa kwa kutumia ujuzi wa ndani, (Local knowledge) katika ubunifu wa majengo (design), upatikanaji wa meneja wa mradi na maandalizi ya kina ya gharama za ujenzi.
Pamoja na pendekezo la kuidhinishwa kwa hatua za ujenzi wa mradi , Baraza pia kupitia Azimio hilo , linamtaka KatibuMkuu kufanya juhudi zote zitakazo pelekea kupunguza muda wa ujenzi wa mradi .
Katika hatua nyingine, Baraza Kuu pia linamtaka Katibu Mkuu kuanza mazungumzo na Asasi nyingine za Kimataifa ikiwamo ile ya Mahakama Afrika itakayoshughulikia Haki za Binadamu, juu ya namna bora ya kushirikiana katika matumizi ya miundo mbinu hiyo katika siku za usoni.
Mwaka 2010 Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha Azimio nambari 1966 la kuanzisha Mfumo wa Kimataifa utakaomalizia Mashauri ya Masalia kwa zilizokuwa Mahakama za Kimataifa za Mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda ( ICTR) na Mauaji ya halaiki yaliyotokea katika iliyokuwa Yugoslavia ya Zamani ( ICTY).
Katika azimio hilo Baraza Kuu la Usalama lilibainisha wazi kwamba Arusha ndiyo itakuwa makao ya Tawi la mfuno huo mpya na The Hague ikiwa ni makao ya Tawi jingine.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2013
(633)
-
▼
April
(40)
- MANGULA NA MALECELA, WAFANYA MAZUNGUMZO
- TASWIRA MBALIMBALI ZA SHEREHE ZA MIAKA 49 ya MUUNG...
- MAONESHO YA NDEGE ZA KIVITA KWENYE SHEREHE ZA MUUN...
- RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA M...
- KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AKUTANA NA BALOZI ...
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU MBAL...
- HABARI ZA MAGAZETINI LEO JUMANNE TAREHE 23TH APRIL...
- PRESIDENT DR. JAKAYA KIKWETE OPENS AU MINISTERIAL ...
- MATUKIO MBALI MBALI YA HITIMISHO YA ZIARA YA KINAN...
- KINANA AICHAMBUA CHADEMA
- CCM YAFUNIKA MKUTANO WA HADHARA MOROGORO JIONI HII
- KINANA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI MORO MJ...
- KINANA KUHUTUBIA WANANCHI WA MOROGORO
- KINANA AFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHA...
- KINANA AONGOZA KIKAO CHA WAKULIMA WA MIWA NA WAMIL...
- KINANA APOKELEWA NA WAFANYA BIASHARA WADOGO MVOMERO
- KINANA AWAPONGEZA VIJANA WA GAIRO KWA KUJISHUGHULI...
- CCM YAWASHA MOTO LEO GAIRO, MKUTANO MKUBWA KURINDI...
- KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA BALOZI WA OMAN NCHINI
- MZEE MWINYI AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI ...
- CCM YAFUNIKA KILOSA, MAMIA WAJITOKEZA KUMSIKILIA K...
- NAPE AWASHUKIA WANASIASA KANJANJA
- NAPE ATOA MAJIBU YA KERO ZA WANANCHI ULANGA
- ZIARA YA KINANA ULANGA, MOROGORO
- MKUTANO WA CCM KILOSA WAFANA
- KATIBU MKUU WA CCM,AWASILI MOROGORO LEO
- RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI BARABARA YA TANGA-HOROH...
- PINDA AFUNGUA SEMINA YA ALBINO DODOMA LEO
- WAZAZI WASIOPELEKA WATOTO SHULE WACHUKULIWE HATUA
- UMOJA WA MATAIFA WAIDHINISHA UJENZI WA MAJENGO YA...
- RAIS KIKWETE AFUNGA SEMINA KWA MAWAZIRI YA UTEKELE...
- RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI WA UKARABATI NA UPANUZI...
- KWA NINI WABONGO HATUPENDI KUJIFUNZA KUTOKANA NA M...
- LOWASSA AWAMWAGIA MAMILIONI YA FEDHA WAISLAM LEO
- SADIFAH ACHANGIA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI VYA VIJANA
- VUAI ASISITIZA KUTUNZA MUUNGANO, Awabeza wanaoupin...
- NAPE AFUNGUA SEMINA YA HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA...
- NAPE ATINGA MKOANI KILIMANJARO LEO, KUUNGURUMA KES...
- JAJI MSTAAFU MWAIPOPO AFARIKI KWA AJALI YA GARI JI...
- UWT YATOA TAMKO, KUHUSU MAJANGA LIKIWEMO GHOROFA 1...
-
▼
April
(40)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.