Google PlusRSS FeedEmail

CCM YAINYONG'ONYESHA CHADEMA WILAYANI MANYONI

NA MWANDISHI WETU
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea kudhihirisha kuwa bado kipenzi cha wananchi, baada ya kukinyong'onyesha Chadema kwa kuzoa viti vingi katika uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji na vitongoji.
     Uchaguzi huo ulifanyika juzi katika vijiji na vitongoji mbalimbali katika wilaya ya Manyoni Vijijini mkoani Singida, ulifanyika kuziba nafasi za viongozi wa ngazi hizo.
     Kwa mujibu wa Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Naomi Kapambala, uchaguzi huo uliofanyika katika ngazi ya vijiji juzi, CCM ilizoa viti 14 na kuiacha kwa mbali Chadema iliyoambulia viti viwili tu kati ya 16 vilivyokuwa vikiwaniwa.
     Naomi alisema kwa njia ya simu kuwa, katika ngazi ya vijiji, CCM ilipita bila kupingwa katika vijiji vinane, huku vinane ulipofanyika uchaguzi ilishinda viti sita.
      Alisema mbali na CCM kutamba kwenye vijiji, pia imeinyong'onyesha Chadema katika uchaguzi katika ngazi ya vitongoji kwa kuzoa viti 35, huku Chadema ikiambulia vitongoji viwili.

This entry was posted in

One Response so far.

  1. Hamadi says:

    Naomba ngazi zote za chama zikutane kujadili masuala makuu yanayoikabili nchi yetu. Masuala hayo ni 1. Ajira, hasa kwa vijana. 2. Utatuzi wa migogoro ya ardhi, hasa vijijini. 3. Mfumuko wa bei. Mikutano hiyo (a) itasaidia ufumbuzi kupatika na (b) kuwaelilimisha wananchi kuwa matatizo ya kiuchumi si matatizo ya Tanzania peke yake bali ni matatizo ya dunia nzima kwa wakati huu.

Leave a Reply