Google PlusRSS FeedEmail

HOJA YANGU NA KAULI YA NASSARI...!

     Inapofikia hali katika nchi ambapo kila mtu yupo tayari kufanya chochote kwa ajili ya mali,wadhifa, madaraka ama sifa ya aina yeyote ile katika jamii.,ni wazi hali hiyo ni ya hatari sana.,lakini kama haitoshi yanapofanywa haya na kuhalalishwa kwa jina lolote lile liwe,uanaharakati,upinzani ama siasa.,hapo ubaya huo uongezeka.,kwani watu watatetea si kwa sababu ni jambo la kulitetea bali kwa kuwa chama changu kimehusika na wala watu hawatapinga ila kwa kuwa chama changu kimepinga.,kwa namna hii tutahalalisha yaliyo haramu na kuharamisha yaliyo halali.


     Kumekuwepo matukio mbalimbali na kauli ambazo kimsingi ni HATARISHI NA CHONGANISHI, mfululizo wa matendo na kauli hizi umeshtua watanzania, wengi wakijiuliza ni nini hatma ya Taifa hili na mwenendo wa kauli hizi za wapinzani. Kauli hizi ambazo wapinzani hasa viongozi waandamizi na wadau wakuu wa CHADEMA wamekuwa wakizitoa kwenye hadhara mbalimbali ambazo kwa upande mmoja unashutumu chama tawala kuhusika katika mauaji ya viongozi wao.

 Chadema wamekuja na mbinu mbaya na chafu za propaganda za kukichafua chama cha Mapinduzi na hata kuwachafua viongozi wake hadharani, na mbaya zaidi kutoa kauli zenye vitisho na zinazopanda mbegu ya ubaguzi na uchonganishi baina ya watu wa Taifa hili kwa mlengwa wa dini zao na kanda. Mara ya kwanza tulizisikia kauli kutoka kwa viongozi waandamizi wakisema kuwa nchi hii haitatawalika, na watafanya kila watachoweza katika kulifanikisha hilo, na mwingine muaasisi wa Chadema wakimshutumu Mwenyekiti baada ya kuunda tume ya Katiba na sasa viongozi wengine wa chama hiki pinzani wananadi hadharani kuwa wataigawa Tanzania na kujitangazia Uhuru kwa upande wa kaskazini kwa mantiki kuwa huko ndiko lilipo chimbuko la Chadema na ndiko ambako chadema inakujali na kujinasbisha nako.

    Matukio ya vurugu ambazo zilitawala kila kona na hata mauaji ni matokeo ya kauli hizi ambazo hazijawahi kukanushwa wala kusahihishwa kwa namna yeyote ile kitu kinachopelekea tuamini kuwa dhamira hii ya viongozi hawa ni ya kweli-hawakukosea kwa ulimi,ni dhamira endelevu.,na wanaifanyia kazi.,bila kujali madhara ya kauli hiyo kwa jamii, ni wazi kuwa hii ni mikakati endelevu ya kuujumu nchi na kufikia malengo yao haya ya kuhakikisha kuwa NCHI HII HAITAWALIKI., kama sivyo kwanini haya hatukuyaona huko nyuma wakati vyama vingine vilipokuwa vyama vikuu vya upinzani.,kwanini sura ya kitaifa imebadilika hivi sasa..,kama ccm ni ile ile tangu kuanza kwa upinzani, sera zake, kanuni na hata katiba ni ile ile basi ni wazi kuwa ni mabadiliko ndani ya upinzani ndio yamezalisha hali hii ya kuchafua sura ya kitaifa hapa nchini kwa kauli na matendo.

    Matendo na kauli za viongozi wa Chadema zinanishawishi kuamini kuwa HAYA YANAYOENDELEA HIVI SASA NI MATOKEO YA MFUMO MPYA NA MBAYA WA UPINZANI WA CHADEMA.,sisemi haya kwa kuwa mimi ni ccm hivyo katika mlengwa wangu kisiasa ni kukipaka matope cdm bali nasema haya kwa ushahidi wa kauli na wa matendo ya waaandamizi na watendaji ama viongozi wa kitaifa wa chama cha chadema . Kauli hizi., hakika ni kauli mbaya sana kuwahi kutolewa na kiongozi wa kisiasa na kitaifa tena ndani ya jukwaa mbele ya halaiki ya watanzania.

Ukiwa Mtanzania mwenye uzalendo na utaifa juu ya nchi hii, laani kauli hii na mfano wa kauli hii ya Nassari. BOFYA HAPA

This entry was posted in

2 Responses so far.

  1. Mwalasha says:

    kiukweli kijana mwenzetu hajielewi.unajua mambo ya siasa yanahitaj kujipanga sasa viongozi waandamiz wa CHADEMA wanatumia vijana kama chambo katika kuupotosha umma wa vijana ambao wengi wao ni taifa la kesho,sasa hali hii ndio inayotokea kwa ndugu Nasari.Nikiwa kama kijana pia nachukua fursa hii kuwashauri vijana waache kupandikizwa mabaya na watu wachache wenye nia mbaya na taifa letu kwa maslahi yao na badala yake kuingia katika chama chenye misingi imara na maslah kwa wote....JIELEWE JOSHUA NA ACHA KUONGEA UJINGA KA UMMA

  2. Kahama says:

    Umechemsha, watanzania sasa hawadanganyiki kwa misemo na kutunga story zisizo na mashiko, chadema hawawezi kuwabadilisha watanzania bali watanzania wamebadilika na dhahili wanahitaji mabadiliko yenye tija kwa nchi na si propaganda

Leave a Reply