Google PlusRSS FeedEmail

RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO BUBUBU,ZANZIBAR HII HAPA

 Halmashauri Kuu ya Taifa katika kikao chake kilichofanyika tarehe 13-14 Mei, 2012 mjini Dodoma, chini ya Mwenyekiti  wake, Mhe. Dk Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na mambo mengine kilipitisha ratiba ya Chama Cha Mapinduzi ya Mchakato wa kumpata mgombea wa kiti cha Uwakilishi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu unaotarajiwa kufanyika Septemba 2012.
Ratiba hiyo imezingatia ratiba ya Tume (ZEC).
1.         RATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI YA MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA WA KITI CHA UWAKILISHI KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA BUBUBU SEPTEMBA 2012
TAREHE
SHUGHULI
26-29/7/2012
Kuchukua na kurejesha fomu ya maombi ya Uongozi wa CCM
30/7/2012
Mkutano Mkuu wa Jimbo la Bububu kupendekeza majina matatu (3).
31/7-4/8/2012
Kampeni ya Matawini
5/8/2012
Kura ya maoni Matawini
6/8/2012
Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Magharibi Unguja
7/8/2012
Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
9/8/2012
Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa
11/8/2012
Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa
13/8/2012
Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa
15/8/2012
Kamati Kuu ya CCM kufanya uteuzi wa Mgombea
.
2.         RATIBA YA TUME (ZEC) YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA BUBUBU
TAREHE
SHUGHULI
22 Agosti -30 Agosti  2012
Uchukuaji na urejeshaji fomu  wagombea
30 Agosti 2012
Siku ya uteuzi wa wagombea
31 Agosti  2012 – 15 Septemba 2012
Kampeni za wagombea
16 Septemba 2012
Siku ya kupiga kura
.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
 ITIKADI NA UENEZI
22/05/2012

This entry was posted in

Leave a Reply