Google PlusRSS FeedEmail

VIONGOZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUA BARABARA YA ARUSHA-NAMANGA-ATHI RIVER

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikata utepe kwa pamoja kuzindua  rasmi wa Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye  urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki  wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River
Viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki Jumatano Novemba 28, 2012 wamefungua rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga kwa upande wa Tanzania, na Namanga– Athi River kwa upande wa Kenya, kama sehemu ya mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi unaofanyika Nairobi, Kenya.
Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye  urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya shughuli za uzinduzi rasmi wa Makao Makuu Mapya za Jumuiya uliofanyika mapema siku hiyo hiyo jijini Arusha, kabla ya viongozi hao kuelekea Athi River kwa ufunguzi wa barabara hiyo.
Ujenzi wa barabara ya Tanga–Horohoro, yenye urefu wa kilomita 66 pia nao umekamilika na  tayari imeanza kurahishisha usafiri na usafirishaji baina ya Tanzania na Kenya na nchi nyingine wanachama.
Barabara nyingine zilizopo katika mtandao wa barabara wa Jumuiya zinazoendelea kujengwa kwa upande wa Tanzania, ni pamoja na zile za mtandao wa Dar es Salaam-Isaka-Lusahunga na Mutukula hadi Masaka; Lusahunga-Nyakasanza hadi Rusumo, na Rusumo-Kigali hadi Gisenyi.
Nyingine ni Biharamulo - Mwanza - Musoma - Sirari - Lodwar – Lokichogio; Tunduma - Sumbawanga - Kigoma - Manyovu (Mugina) - Rumonge - Bujumbura - Ruhwa (Bugarama) – Karongi hadi Gisenyi, pamoja na ile ya Tunduma - Iringa – Dodoma - Arusha - Namanga hadi Moyale.
Ujenzi wa barabara hizi utarahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na huduma baina ya nchi wanachama, na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji na vilevile gharama za kufanya biashara katika nchi za Jumuiya na hivyo kuvutia uwekezaji.

This entry was posted in

Leave a Reply