Google PlusRSS FeedEmail

ZIARA YA KINANA SUMBAWANGA, AHUDHURIAA KIKAO CHA SHINA

Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Chipukuizi wa CCM, wakati wa mapokezi yake kwenye Uwanja wa Ndege wa  Sumbawanga mkoani Rukwa, alipowasili mkoani Rukwa, jana, akiwa katika ziara yake ya siku nne kujitambulisha, kukagua na kueleza kwa wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika mkoa huo na mikoa ya Mtwara, Geita na Arusha.  (Picha zote na Bashir Nkoromo)

Kinana akimsalimia Mwanasiasa mkongwe, Chrisant Mzindakaya, kwenye Uwanja wa Ndege wa sumbawanga, mkoani Rukwa, jana

Wajumbe wa mkutano wa shina namba moja la Kisesa mkoani Rukwa wakimsikiliza Kinana wakati akiwahutubia, aliposhiriki mkutano wao uliofanyika jana.


Wana-CCM wakiwa na bango la kumpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdylrahman Kinana, mpongeza Kinana katika mkutano uliofanyika jana Sumbawanga mjini mkoani Rukwa


Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggry Mwanri  akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jana mjini Sumbawanga


 Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatib akisalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mjini Sumbawanga mkoani Rukwa

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nape akihutubia  mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jana mjini Sumbawanga (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)

This entry was posted in

Leave a Reply