Google PlusRSS FeedEmail

CCM YAPIGA KIPYENGA KALENGA; MWIGULU AMNADI MGOMBEA WA CCM ADAI DK. SLAA ANA MAPEPO ZAIDI YA SABA KICHWANI

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa, alipozindua rasmi kampeni za CCM jioni hii katika mapnei za CCM zilizofanyika Uwanja wa Ifunda, Iringa Vijijini.(Picha na Bashir Nkoromo)

Mwigulu:Slaa ana mapepo

Na Mwandishi Wetu, Kalenga, Iringa

NAIBU Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mwigulu Nchemba amesema kichwa cha Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Willibrod Slaa kina mapepo zaidi ya saba.

Amesema Dk.Slaa baada kuacha kumtumikia Mungu mawazo na mtazawamo wake amekuwa ni mtu wa kuzusha uongo.

Mwigulu alitoa kauli hiyo jana kijiji cha Ifunda katika Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa wakati akizindua kampeni za uchaguzi mdogo wa chama hicho.

CCM imemsimamisha mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na mbunge wa jimbo la Kalenga Dk.William Mgimwa, Godfrey Mgimwa kugombea nafasi ubunge kujaza nafasi iliyoachwa wazi.

Alisema kuwa Biblia inasema kuea mtumishi wa Mungu atakayerudi nyuma atakuwa na mara sabini, na hicho ndicho kinachotokea kwa Dk.Slaa.

"Ndio maana hivi sasa ana miaka 70 lakini anamchumba, mate yake yamejaa uongo.Amezoea kusema uongo na kufanya maandamano.

"Kazi ya Dk.Slaa ni kusema uongo kila siku.Na tabia yake ya kufanya maandamano imefika mahali hata akilala usiku anamka na kuanza kuzunguka kitanda maana anafanya maandamano hadi nyumbani kwake,"alisema.

Aliongeza kuwa leo hii akitakiwa kutaja jina la mtu mmoja nchini ambaye hamuheshimu basi atataja jina la Dk.Slaa na hiyo inatokana na tabia yake  ya kusema uongo na kutukana kwenye majukwaa.

Hata hivyo, alisema kuwa Dk.Slaa anahangaika kwasababu kila mwisho wa mwezi analipwa sh.milioni saba , hivyo kinachomfanya kuzungumza ni kufanikisha maslahi yake na wenye uchunguzi na wananchi ni Serikali ya CCM.

Wakati huo huo,Mwigulu alisema kuwa  wenye kutaka nyongeza ya posho katika Bunge la Katiba wanajisumbua huku akisisitiza anayeona haitoshi aondoke.

Alisema yeye akiwa Naibu Waziri wa Fedha, hawezi kukubali kuona posho inaongezwa na huku akisisitiza atakuwa makini kusimamia matumizi mazuri ya fedha za Serikali.

Alisema kabla ya kuwa Naibu Waziri amekuwa akikerwa na tabia ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali na ndio maana aliamua kukemea hata kitendo cha  Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kumshinikiza mbunge wa viti maalumu wa chama chake aende Dubai kwa kazi maalumu,"alisema Mwigulu.


Amesema kuwa Dk.Slaa anahangaika kwasababu kila mwisho wa mwezi analipwa sh.milioni saba , hivyo kinachomfanya kuzungumza ni kufanikisha maslahi yake na wenye uchunguzi na wananchi ni Serikali ya CCM.

Mwigulu alitoa kauli hiyo jana kijiji cha Ifunda katika Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa wakati akizindua kampeni za uchaguzi mdogo wa chama hicho.

Alisema kuwa CCM ndio yenye Ilani inayotekelezwa ambayo wananchi waliingia mkataba na chama hicho na kinachoendelea sasa ni utekelezaji wake.

"Tunahitaji maendeleo ya wananchi, tunazungumzia mambo ya msingi kwa ajili ya maisha ya wananchi wa Kalenga.Huyu Slaa anahangaika kwasababu anahitaji kulipwa mwisho wa mwezi.


"Huwa nashangaa watu wanaoshabikia Chadema, maana hawana wanachofanya zaidi ni kutengeneza makesi kila siku.Fuatilia wabunge wanaume tabu na wanawake nao tabu

Hata hivyo alisema uchaguzi huo si wa kupambanisha sera maana ni uchaguzi mdogo na kwamba uchaguzi mkuu mwaka 2010, tayari Watanzania waliingia mkataba na CCM.

Alisema kuwa ilani ya inayotekelezwa sasa ni ya CCM na upinzani hauna wanachotekeleza na hata kusimamia mgombea wao ni ushamba wa siasa.

"Kinachoendelea sasa ni kutekeleza maendeleo kupitia ilani ya CCM ambayo wanayoimiliki ni wa CCM.Hivyo hakuna sababu ya kupoteza muda,"alisema.

Alisema, umefika wakati kwa wananchi kumtuma kijana Godfrey Mgimwa ili akafanye kazi ya kuleta maendeleo yao na si kuchagua mbunge kwa sababu tu ya kuchagua.

Hata hivyo, alisema wananchi wanahitaji barabara, maji, umeme afya bora na huduma nyingine za msingi na mwenye kufanya kazi hiyo ni Serikali ya CCM, hivyo Mgimwa atasaidia katika kufanikisha hilo.

Aliongeza kazi ya upinzani ni kuomba jamii ipate matatizo ili wao wapate nafasi ya kusema .Haiwezekani kuwa na wanasiasa ambao kazi yao ni kuombea matatizo kila siku.

Mwigulu aliwaomba, wananchi kuacha ushabiki katika mambo ya maendeleo, hivyo hawatakiwi kufanya kosa kwa kumchagua mtu ambaye anatoka nje ya CCM.

Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Iringa Dk.Pindi Chana alisema kuwa wananchi wanahitaji maendeleo na si maandamano.

Alisema anashangazwa na Chadema wanashindwa kutatua matatizo ya wananchi na badala yake wanazunguka hewani kwa helkopta wakati wananchi wapo chini.


Akizungumza katika mkutano huo, Chifu wa kabila la Wahehe,Abdul Mkwawa alisema kuwa kamwe hawezi kuwa Chadema na wanaozusha kuwa amemkaribisha Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Willibrod Slaa katika Jimbo la Kalenga wanajisumbua.

Alisema kuwa yeye ni kada wa CCM na ataendelea kuwa chama hicho na kwamba damu yake ni CCM.

"Siwezi kuwa Chadema wamezusha hadi kwenye mitandao eti nimemkaribisha Slaa Kalenga na wanadai mimi ni Chadema.Si kweli kwanza huyo Slaa wa kazi gani huku kwetu,"alisema.


Katibu CCM Wilaya

Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini Hassan Mtaturu alisema kuwa wafuasi na wanachama wa Chadema wameanza kufanya vurugu lakini alionya kuwa hatawakuwa tayari kuvumilia.

Alisema kuwa watadhibiti na katika hilo hawatakuwa na huruma maana hawapo tayari kuonewa.

Alisema tayari wamepata majina ya vijana wa watu wa Chadema ambao wamebainika kufanya hujuma dhidi ya CCM ambao waliamua kuweka vibao vyenye misumari ili magari yaliyokuwa na wanachama wao yaharibikie.

Alitaja majina ya vijana waliotega misumari hiyo Issa Nyamahanga , Martin Nyangi na Rashid Dau wote wa Kijiji cha Wasa.

"Tumeanza uchunguzi , hivyo majina hayo tutakabidhi polisi ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa hatua.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Nsambatavangu alisema kuwa Chadema si chama ambacho kinastahili kupewa nafasi kwani kazi yake ni kuvuruga amani ya nchi.

Alisema kuwa kazi yao imekuwa kumtukana Rais , Serikali na CCM huku muda mwingi wakitumia kuhamasisha vurugu na maandamano.

Alisema wananchi wa Kalenga wasifanye makosa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kwa kuchagua mtu ambaye atakuwa ni wa vurugu kila kukicha na badala yake wachague CCM kwa maendeleo.

This entry was posted in

Leave a Reply