Google PlusRSS FeedEmail

SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM MAREKANI KUFANYIKA LEO JUMAPILI

NA MWANDISHI MAALUM NEW YORK
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la DMV zitafanyika Sherehe za Miaka 37 ya CCM leo, Jumapili, Feb 23, 2014 kwa shamrashamra, hoi hoi na vikolombwezo kibao.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Tawi hilo, Salma Mosha, sherehe hizo, zitanogeshwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Bal;ozi Liberata Mulamula ambaye ndiye amepangwa kuwa mgeni rasmi.

Amesema, shamrashamra hizo zitafanyika Hampton Inn 9670 Baltomnore Ave Collage Park MD 20740, kuanzia saa kumi jioni.

"Katika sjereje jizi tutatoa fomu kwa wanachama wanaotaka kuwania nafasi ya ukatibu. Karibuni wanachama wa CCM na Watanzania wote kwa jumla", amsema Salma katika taarifa hiyo.

This entry was posted in

Leave a Reply