Google PlusRSS FeedEmail

HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA YAENDELEA LEO



 Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe wa NEC wakati wa ufunguzi wa kikao cha NEC ambacho kinaendelea leo mjini Dodoma , kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakipitia magazeti yalotoka leo Februari 16,2014 kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma ambacho leo kinategemewa kumalizika.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Steven Kazidi kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma leo Februari 16,2014.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM(Bara) Ndugu Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na wajumbe wa NEC Ndugu Said Nkumba na Jestina Mhagama kabla ya kikao cha NEC akijaanza mjini Dodoma.
 Pichani ni Wajumbe wa NEC kutoka Zanzibar Dk.Maua Daftari na Asia Sharif wakati wa kikao cha NEC kinachoendelea mjini Dodoma ambapo moja ya mambo yanayojadiliwa ni Rasimu ya Katiba.
 Wajumbe wa NEC kutoka Kusini Unguja Ndugu Ramadhani Abdala Shabani na Ndugu Mussa Makame  maarufu kwa jina la Dere wakizungumza nje ya ukumbi wa NEC kabla ya kikao hakijaanza.
Profesa Mark Mwandosya akizungumza na Godfrey Zambi nje ya ukumbi wa NEC kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC ambacho kinatarajiwa kumalizika leo mjini Dodoma.

This entry was posted in

Leave a Reply