Google PlusRSS FeedEmail

SALMA MOSHA: BALOZI ZINA NAFASI KUBWA YA KUTANGAZA UTAMADUNI WA TANZANIA KIMATAIFA

NA MWANDISHI MAALUM, USA
Msanii mkongwe wa kuchezea nyoka, Salima Moshi, amesema Balozi zina nafasi nzuri  za kuutangaza utamaduni wa Tanzania nje ya nchi kwa kuwa wapo karibu na nchi husika.

Amesema kutokana na ukaribu huo mabalozi wanaweza kujenga mazingira ya kuviwezesha vikundi kwenda kufanya maonyesho katika nchi hizo za nje.

Salma amesema hayo alipokwenda kumuona Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Liberata Mulamula, kwa ajili ya kumsalimia na kuwa na mazungumzo.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anaishi Marekani, pia aliomba BARAZA LA SANAA LA TAIFA  kuandaa kitabu kitakachojumuisha wasanii mbalimbali na anwani zao vitabu hivyo vipelekwe kwenye balozi zetu ili watu mbalimbali wanaokuja waweze kuvisoma na hatimaye kuwaalika wasanii wataweza kuutangaza utamaduni wetu na wasanii kujipatia kipato na pia kujifunza.

Alisema mapromota wengi baada ya kupata wamekuwa wanawatelekeza wasanii na pato kubwa linaenda kwao bila kunufaisha msanii  na hata wale wanaobahatika kupiga sanaa zao nje ya Tanzania wamekuwa wanaishia kuwapigia Watanzania ifike wakati wakiwa nchi za nje waweze kutumbuiza na wenyeji  huku akitoa mfano kama JZ aende Tanzania halafu awapigie Wamarekani.

Salima alikemea vikali swala la kukopi kazi za sanaa linarudusha nyuma maendeleo ya wasanii na aliomba Serikali kutoa adhabu kali kwa watakao bainika na kusimamia swala la hakimiliki.

Msanii huyo mkongwe alisema imefika wakati sasa wasanii kuwa na wanasheria hali ambayo itasaidia kulinda haki zao.

Salima alimshuru sana Rais Jakaya Kikwete akisema amekuwa wakati wote karibu na wasanii  na hata hivi karibuni aliwaalika kwenye  chakula cha jioni na kuomba nafasi hiyo wasanii waitumie vizuri.

Alisema kuhusu tunzo   ziwe zinatoa kwa wasanii   wa sanaa za maonyesho   na wakati umefika kutoa kibali kwa waandaaji wengine si vibaya zikawa zaidi ya moja  pia aliombakusaidia kujenga maktaba  kwenye eneo la viwanja vya wasanii Mkuranga na kumpongeza Mwenyekiti wa wasanii bw Twalibu.

Balozi Mulamula alimshukuru sana msanii huyo na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuwakilisha nchi na kuwa msanii atakayekuwa mfano kwa wengine.

Alisema kuhusu Hakimiliki  Serikali imejizatiti kikamilifu  kuhakikisha haki za msanii zinalindwa alisema ni vyema wasanii wakajua haki zao hii itawasaidia sana  aliongolea mapromota ni vyema kuangalia maslahi ya wasaniikwanza MH Balozi alisifu sana kazi zinazofanywa na wasanii mbalimbali nchinina kuitangaza nchi

 Msanii wa siku nyingi wa kuchezea nyoka, Salma Mosha (kushoto) akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Mrekani, Balozi Liberatha Mulamula, alipoenda kuzungumza na balozi hiyo ofisini kwake nchini Marekani.

This entry was posted in

Leave a Reply