Google PlusRSS FeedEmail

MAREKANI WAMLILIA TAMBALIZENI

Chama Cha Mapinduzi (CCM)- DMV, kimesema wanachama wake wamepokea kwa msituko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Kada wa CCM na msanii maarufu Tanzania, marehemu  Salum Tambalizeni aliyefariki juzi nyumbani kwake, Kiwalani Minazi Mirefu, Dar es Sakaam na kuzikwa jana katika makaburi ya Malumbo, Kisarawe mkoa wa Pwani.

Taarifa iliyotupwa na Katibu Mwenezi wa CCM tawi la DMV, Mama Salma Mosha imesema, Marehemu Salum Tambalizeni alikuwa Kada mwenye muono na msanii ambaye alikuwa anajituma sana na kuonyesha mfano mzuri kwa wasanii wengine.

"Niliona kipaji chake, nikamuingiza kwenye kikundi cha DDC Kibisa, kwenye miaka ya 80, niliweza kupata nafasi Radio Tanzania (sasa TBC Taifa),  na ngonjera zake kutoka kila siku. kutoka hapo aliweza kushika nafasi mbalimbali kwenye Chama.", alisema Salma Mosha ambaye pia ni msanii wa siku nyingi wa kuchezea nyoka ambaye sasa anaishi nchini Marekani.
Mama Salma Mosha

Alisema, wana-CCM wa Marekani wanatoa pole kwa CCM mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa jumla, wasanii wote, ndugu na jamaa wa marehemu na kuwaomba kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu.

"Tunamuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi" Ameni.

This entry was posted in

Leave a Reply