Google PlusRSS FeedEmail

MTENDAJI KISHAPU, ADAIWA KUKWAPUA MAGUNIA 103 YA MAHINDI YA NJAA YALIYOTOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

SHINYANGA, Tanzania 
MKUU wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga  Wilson Khambaku  amemsimamisha kazi  mtendaji  wa kata  ya Bubiki tarafa ya Mondo  anayetuhumiwa kuiba magunia 103 ya  mahindi  yaliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa  kwa msaada wa kusaidia  chakula  kaya masikini  kata hiyo.

Mkuu huyo aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Busangwa  na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa kata hiyo,ambapo alitoa kauli ya mtendaji huyo aliyefahamika kwa jina la Boniface Charles  ashitakiwe na kupelekwa mahakamani huku uchunguzi  zaidi ukiendelea kwa wengine walioshirikiana nae.

Hatua ya kumsimamisha kazi na kuagiza akamatwe na kufikishwa mahakamani alisema kuwa  tuhuma hiyo  katika uchunguzi uliofanywa  na  jeshi la polisi kitengo cha upelelezi wilayani humo  imeonekana mtendaji wa kata  hiyo kuhusika  kwa kushirikiana na baadhi ya watu wengine.

“Wananchi msiwe na wasiwasi  tutawakamata tu,hatua zitakazochukuliwa  na kamati ya maafa ya wilaya ni kuagiza uchunguzi ufanyike dhidi ya viongozi wasiokuwa waadilifu wanaohusika  na upotevu  wa  mahindi ya msaada  magunia 103 ikiwa kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika leo  mtendaji huyo inaonekana anahusika.”alisema  Nkhambaku.

Jeshi la polisi linaendelea kuwasaka wale wengine walioshirikiana na mtendaji wa kata ili nao waweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hiyo.

Mkuu huyo aliwahakikishia  wananchi hao kuwa  serikali ipo makini  na kuwatoa hofu kwa kupata msaada wa mahindi mengine kama mgao ulivyopangwa ingawa tayari imeonekana kupata hasara dhidi ya upotevu wa mahindi hayo.

Baadhi ya wakazi waliohudhuria mkutano huo John Shija na Soseja  Maduhu walisema kuwa mahindi ya msaada  waliyaona  yakishushwa katika ofisi ya kata lakini hawakuona yamegawiwa wapi kadri siku zinavyozidi kwenda huku kaya zikiendelea kulala na njaa  na kufikiri mahindi hayo yalikuwa siyo yao bali yaliwekwa kuhifadhiwa.

This entry was posted in

Leave a Reply