Google PlusRSS FeedEmail

UFOO SARO APIGWA RISASI DAR ES SALAAM

DAR ES SALAAM, Tanzania
Mtangazaji wa ITV, Ufo Saro amepigwa risasi na kijana Ateri Mushi anayesemekana kuwa alikuwa mume au mchumba wake.

Taarifa zilizopatikana zimesema, kijana huyo pia amempiga risasi ya kifuani mama mzazi wa Ufoo na kufa papo hapo katika tukio hilo lilifanyika leo alfajiri nyumbani kwa Ufoo, Kimara, Dar es Salaam.

Imeelezwa kwamba hadi sasa Ufoo yupo katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akipatiwa matibabu.

Kulingana na taarifa hizo, kijana huyo baada ya mashambulio hayo dhidi ya Ufoo na mama yake, naye alijipiga risasi na kufa papo hapo.

Ufoo Saro akiwa na Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, nyumbani kwa Mama Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam mwaka jana.

This entry was posted in

Leave a Reply