- Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ameongoza mamia ya wakazi wa Dar Es Salaam na mkoa wa Pwani katika mazishi ya Kada na Mshairi maarufu wa CCM salum Tambalizeni yaliyofanyika Marumbo Kisarawe.
- Pia atoa heshima za mwisho kwa Kada wa CCM na kiongozi wa wazazi Tawi la Mbuyuni kata ya Kigogo,Marehemu Clemence Ndaghala aliyefariki tarehe 10 Oktoba katika hospitali ya muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kisarawe Ndugu Tatu Kana leo Marumbo Kisarawe kabla ya mazishi ya Kada na Mshahiri wa CCM Salum Tambalizeni.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa salaam za pole kwa wafiwa kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi na salaam za Mwenyekiti wa CCM Taifa, ambapo alimwelezea Tambalizeni kuwa alikuwa mtu wa kupenda kusaidia watu na kushiriki kwenye masuala ya maendeleo ya watu waliomzunguka,aliendelea kusema si rahisi pengo lake kuzibika.
Mwili wa marehemu Salum Tambalizeni ukipelekwa makaburini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kutia udongo kwenye kaburi la Marehemu Salu Tambalizeni.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixts Mapunda akishiriki kutia udongo wakati wa mazishi ya Salum Tambalizeni yaliyofanyika Marumbo Kisarawe.
Ndugu,Jamaa na Majirani wa Clemence Ndaghala wakipokea neno takatifu kabla ya kuanza kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Clemence Ndaghala aliyefariki tarehe 10 Ocktoba katika hospitali ya Muhimbili.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Clemence Ndaghala aliyefariki tarehe 10 Oktoba kwenye hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.