MBUNGE MAJI MAREFU ANAPODAIWA KUSAKWA KWA WIZI WA GARI LA WAZIRI
Stori hiyo iliyochapwa katika gazeti la Uwazi, juzi, ilimhusisha Mbunge wa Korogwe Vijijini, Profesa Maji Marefu akidaiwa kusakwa na Polisi kwa tuhuma za wizi wa gari la Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mbunge wa Mvomelo Amos Makalla.
Kutokana na stori hiyo kuonyesha kuwa ya mvuto wa aina yake kutokana na kuwa ya kijamii, huku ikisababisha maswali mengi ya kwa nini ilitokea, tunaileta tena kwenu wadau kama ilivyotayarishwa na theNkoromo Blog, ili wale ambao hawakupata fursa ya kuisoma kwenye gazeti muweze kuisoma kama ilivyo ada uwanja wa maoni kwa atakayekuwa nayo kuhusu stori hii upo wazi....