Google PlusRSS FeedEmail

BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO MJINI DODOMA

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira akiwaeleza jambo wajumbe wenzie Bi. Anna Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Richard Ndassa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sumve, kabla ya kuingia katika Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi John Magufuli akimweleza jambo Mjumbe mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo Bw. John Mnyika Mapema leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Ismail Aden Rage (mwenye kanzu) na Hashim Rungwe wakielekea katika ukumbi wa Bunge mapema leo Mjini Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwaeleza jambo wajumbe wa Bunge maalum la Katiba Edward Lowassa (mwenyeshati Jeupe) na Philemon Ndesamburo, Ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mufti, Sheikh Thabit Noman Jongo akiongoza  dua ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Askofu Mstaafu Donald Mtetemela akiongoza sala ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.(PICHA NA HASSAN SILAYO)

This entry was posted in

Leave a Reply