Google PlusRSS FeedEmail

KIONGOZI UVCCM AFUNGA TAWI LA CHADEMA NA KUPANDISHA BENDERA YA CCM-LUSHOTO


 Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko akiwa ameshika Bendera ya Chadema baada ya wanachama wote wa Tawi hilo kurudi CCM katika Kijiji Cha Lukozi na kupandisha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza Ufalme mpya wa Chama hicho cha siasa.
 Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko akipandisha Bendera ya CCM mahala ambapo kulikuwa na  tawi la Chadema  katika Kijiji Cha Lukozi na kupandisha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza Ufalme mpya wa Chama hicho cha siasa.



Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko amefunga tawi la Chadema katika Kijiji Cha Lukozi na kupandisha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza Ufalme mpya wa Chama hicho cha siasa.

Tukio hilo limetokea jana tarehe 6th March 2014 katika kijiji cha Lukozi, wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga, ambapo sambamba na kuasisi tawi hilo la Chama Cha Mapinduzi pia kiongozi huyo wa UVCCM ameingiza wanachama wapya 206 ambapo wengi wao walikuwa ni wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Mjumbe huyo wa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM, alifungua mashina sita yakiwemo ya Manyara, bodaboda, n.k pia alifanya vikao vinne vya ndani ambapo alizungumza na wanaCCM juu ya hali ya Uimara wa Chama na kuhoji kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Kijiji hicho ndani ya Wilaya ya Lushoto pamoja na kufanya mkutano wa hadhara ambao ulihudhuriwa na wananchi wengi wa Lukozi.

Pamoja na vikao hivyo lakini pia Husna alitembelea vikundi vya ujasiriamali vya  akinamama pamoja na kambi ya JUDO ya Vijana wilayani Lushoto na kujadili nao Changamoto wanazokutana nao na kushirikiana nao kuzipatia ufumbuzi.

Husna anafanya ziara za kawaida katika Mkoa mzima wa Tanga katika kuhamasisha Vijana kujiunga na Chama Cha Mapinduzi pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Vijana.

This entry was posted in

Leave a Reply