Google PlusRSS FeedEmail

SILAA AMNADI MGOMBEA WA CCM KALENGA, LEO

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na mjumbe wa Kamati kuu ya Chama chama Mapinduzi (CCM) Bw. Jerry Silaa kulia akiteta jambo na Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Bw. Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha ibumila kata ya Mgama halamashauri ya wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa, Jerry Silaa amewaomba wana Ibumila kumchagua Godfrey Mgimwa ili kukamilisha mipango mbalimbali aliyoiacha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Marehemu Dk. William Mgimwa. 2 
Mmoja wa wananchi akiserebuka huku akiwa amebeba beseni lake la ndizi katika mkutano huo. 5 
Wananchi wakimlaki mgombea ubunge wa Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa wakati alipowasili katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama. 9 
Jeshi la polisi likiimarisha ulinzi katika mikutano hiyo 10 
Kada wa chama cha Mapinduzi Bw. Fredrick Mwakalebela akipigia debe mgombea ubunge wa jimbo la Lalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo leo.
 13 
Mgombea ubunge wa jimbo la Lalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa akivishwa mgorole na wazee wa kimila kama ishara ya heshima mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo leo.

This entry was posted in

Leave a Reply