Google PlusRSS FeedEmail

MKUU WA WILAYA HANANG AVALIA NJUGA UJENZI WA MAABARA KATIKA KILA SHULE YA SEKONDARI WILAYANI HUMO


HANANG, Tanzania
Serikali ya wilaya ya Hanang ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Christina Mndeme, imeanza kutekeleza ujenzi wa maabara katika kila shule ya sekondari wilayani humo, ili kukabiliana na upungufu wa watalaam wa sayansi.

Mkuu wa wilaya Christina Mndeme, ameagiza kila shule ijenge vyumba vitatu vya maabara ambapo masomo ya Fizikia, Kemia na Bailojia yatatumika kwa vitendo.

Mkuu huyo wa wilaya ameagiza ifikapo June 30 mwaka huu, shule zote 31 kati ya 33 zenye upungufu wa maabara ziwe zimekamilisha ujenzi wa vyumba kwa nguvu za wananchi na serikali itamalizia.

Amewaagiza watendaji wote wa kata kuunda kamati za ujenzi wa maabara za kata na vijiji na pia ameunda kamati ya maabara ya wilaya ambayo itafanyakazi chini ya uenyekiti wake mkuu huyo wa wilaya.

Amesema lengo la wilaya ni kuwa ifikapo Mwishoni mwa mwaka huu wa 2014, wanafunzi wote wakidato cha nne katika mtihani wao wa taifa wafanye kwa vitendo.

"Uwepo wa maabara utachochea kasi ya wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na hivyo kuongeza watalaam wa sayansi wakiwemo Walimu, maafisa ugani, madaktari, manesi", Mkuu huyo wa wilaya alisema alipokuwa akitoa agizo hilo hivi karibuni wakati akiozungumza na watalaam wa Halmashauri ya wilaya yake.

This entry was posted in

Leave a Reply