Google PlusRSS FeedEmail

MANGULA AISIMANGA CHADEMA KALENGA, ASEMA CCM LAZIMA ISHINDE


Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na viongozi wa CCM katika kata ya Mgama kijiji cha Mgama mara baada ya kuwasili kjijini hapo kwa ajili ya kufanya mkutano na wajumbe wa harmashauri kuu ya Kata hiyo ili kujadili kwa pamoja mwennendo wa kampeni katika jimbo la Kalenga ambapo chama hicho kimemsimamisha Bw. Godfrey Mgimwa kuwa mgombea wa jimbo hilo, uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Machi 16 mwaka huu. 2Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akishiriki kuimba wimbo na wana CCM mara baada ya kuwasili katika kikao hicho cha ndani kilichofanyika kwenye kijiji cha Mgama. 3Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akishiriki kucheza ngoma kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa ndani uliofanyika leo kwenye kijiji Mgama 4Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akifurahia jambo kwa kupiga makofi wakati wa mkutano huo wa ndani kulia ni Mwenyekiti wa CCM Iringa Vijijini mama Delfina Mtavilalu. 5Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akizungumza na waandishi wa habari kijijini Mgama mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa ndani. 6Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisoma mambo muhimu yanayohusu uchaguzi huo kwa wana CCM. 7Baadhi ya viongozi wa CCM katika ngazi ya vijiji na kata wakiwa katika mkutano huo 8Msafara wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula ukiwasili katika kijiji cha Mgama 9Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa ndani
................................................................................................
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amekifananisha chama cha CHADEMA sawa na wachuuzi wa biashara za mkononi (wamachinga) kwa kutokuwa na maeneo rasmi ya kuendesha shughuli zao.  Mangula amesisitiza kuwa CCM imejipanga na ina uhakika wa kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa vijijini. Kiongozi huyo wa juu wa CCM aliyasema hayo jana katika kijiji cha Mugama kata ya Mugama wilayani humo wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya kata hiyo. Mangula alitoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi huo katika kata ya Mugama ambapo Katibu wa CCM kata ya Mugama Sylvester Samon kueleza kuwa chama cha CHADEMA ambacho ni mshindani wa CCM katika uchaguzi huo hakina dalili kushinda. Samson alisema CHADEMA haina ofisi hata moja katika kata nzima ya Mugama jambo linalokitia hofu chama hicho na kulazimika kutumia mbinu chafu ikiwemo kushusha bendera za CCM na kuchana mabango ya mgombea wake. Baada ya kuelezwa hayo, Mangula alisema CHADEMA kimekosa mwelekeo ndani ya kata hiyo na jimbo zima la Kalenga kwa kuwa kimekuwa sawa na wamachinga kwa kutokuwa na na ofisi ambazo ni dalili ya kukubalika na kuwa na wanachama kwenye eneo husika. “CHADEMA hakina hata ofisi moja katika kata nzima, hivi unaweza kusema kina dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwenye eneo hili au wanataka kuwalaghai na kuwarubuni wananchi,” alisema. Alisema CCM imejipanga kupata ushindi wa kishindo kutokana na mafanikio na utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambapo mambo mbalimbali ya maendeleo yamefanikiwa kutekelezwa. Kwa mujibu wa Mangula, uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi ya mbunge wa CCM hivyo ni vyema wana-Kalenga wakamrudisha mwana-CCM ili akamilishe ahadi zilizotolewa na Chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Mugama, Betha Luhavi, alisema Chama kina taarifa kamili kuhusu wapiga kura wa eneo hilo hivyo hakuna mtu kutoka nje ya eneo hilo atakayepewa nafasi ya kujipenyeza ili kuvuruga uchaguzi huo. Betha alisema hadi sasa tayari CCM imefanikiwa kuyazunguukia matawi yote yaliyo kwenye kata hiyo kwa lengo la kuhamasisha makada na wapenzi wake siku ya kupiga kura wajitokeze kupiga kura. Alisema viongozi na wapenzi wa CCM watakuwa mstari wa mbele kuhamasisha amani kipindi chote cha kamepeni na siku ya uchaguzi ili kuhakikisha ubnafanyika kwa amani. Aidha, alisema CCM itashirikiana na vyombo vya dola kufichua uhalifu wa aina yoyote unaolenga kuvuruga uchaguzi na amani katika kata hiyo na jimbo la Kalenga kwa jumla. Uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kalenga unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu ambapo CCM imemsimamisha Godfrey Mgimwa kuwa mgombea wake atakaechuana na wagombea wengine. uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake Dk. William Mgimwa kufariki dunia Januari mwaka huu wakati akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini. PICHA NA HABARI NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KALENGA

This entry was posted in

Leave a Reply