Google PlusRSS FeedEmail

TAKWIMU RASMI NA ENDELEVU NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA SERA ZA MAENDELEO -UMOJA WA MATAIFA

Mkurugenzi Mkuu, Idara Kuu ya Taifa ya  Takwimu Dkt. Albina Chuwa anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 45 wa Kamisheni ya  Takwimu ya Umoja wa Mataifa,  akifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo wa wiki moja Unaofanyika   hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya nchi 24  ambazo ni Wajumbe wa  Kamisheni hiyo. Mkutano wa Kamisheni  ulifunguliwa na  Bw. WU HONGBO, Katibu Mkuu Msaidizi  anayeongoza Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na  Maendeleo ya Jamii ( ECOSOC)   Katika Hotuba yake  Bw. HONGBO ametoa changamoto kwa wataalamu hao wa Takwimu  ya kuhakikisha kwamba wanafuatilia kwa karibu  majadiliano yanayoendelea kuhusu ajenda mpya za maendeleo endelevu baada ya 2015 kwa kile alichosema, utekelezaji wa malengo hayo  utahitaji kuungwa mkono na takwimu rasmi na endelevu.
  Na  Mwandishi Maalum, New Yok
Wajumbe  wanaohudhuria  Mkutano wa 45 wa Kamisheni ya  Takwimu ya Umoja wa Mataifa, wamepewa changamoto ya kuhakikisha kwamba, Takwimu rasmi na sahihi zinaunga mkono pamoja na  mambo mengine, utekelezaji  na  usimamizi wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) baada ya 2015.

Changamoto hiyo imetolewa siku ya Jumanne na  Katibu Mkuu  Msaidizi Bw. WU HONGBO anayeongoza  Baraza la Umoja wa Mataifa  linalosimamia masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii ( ECOSOC). Bw. HONGBO alikuwa akifungua rasmi mkutano wa wiki moja wa wajumbe  wanaounda Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa.

Wajumbe hao ni kutoka nchi 24 ikiwamo  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ujumbe wake  katika Mkutano huu  unaongozwa na  Dkt. Albina Chuwa,  Mkurugenzi Mkuu wa Idara  Kuu ya Taifa ya Takwimu.

Bw. WU HONGBO amewaeleza  wataalamu hao wa masuala ya Takwimu kwamba,  mwezi wa Tisa mwaka huu,  Umoja wa Mataifa, utaandaa mikutano kadhaa ya  kilele, ukiwamo  Mkutano wa Tatu wa Kimataifa kuhusu maendeleo ya  mataifa ya visiwa  vidogo.

Ni katika kipindi hicho hicho pia ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amewaalika Wakuu wa Nchi na Serikali,    wafanyabiashara,  vyama visivyo ya kiserikali, na watu wa kada mbalimbali kuhudhuria mkutano  wa kilele kuhusua masuala ya  mabadiliko ya Tabia nchi.

“ Hivi sasa kuna mchakato  unaoendelea  wa majadiliano  ya  wazi ya  Kikundi Kazi kuhusu ajenda mpya za Malengo  ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015 ( SDGs).

Majadiliano haya na mengine , ni wazi kwamba  nafasi na mchango wa Takwimu  ni  muhimu sana katika kuchangia na kutoa mwongozo wa uundaji wa  será na  uundwaji wa  kamati za ufuatiliaji wa utekeleazaji wa makubaliano yatakayofikiwa” akasisitiza Katibu Mkuu  Msaidizi.

Katika  kuhakikisha kwamba,  wataalamu hao  kutoka Taasisi za Kitaifa za Takwimu wanafuatilia  kwa karibu  mikutano  mbalimbali  muhimu inayoendelea  katika Umoja wa Mataifa,  yakiwamo majadiliano ya Kikosi   Kazi kuhusu  Maendeleo Endelevu baada ya 2015.

Katibu Mkuu Msaidizi, Bw. HONGBO amesema, wakati mkutano huo wa Kamishieni ya Takwimu ukifanyika,  katika ukumbi mwingine,  kulikuwa kukiendelea  majadiliano ya awamu ya tisa kuhusu  maendeleo endelevu baada ya 2015.


“ Wiki hii inatoa fursa ya aina  yake kwenu,  pamoja na ajenda mbalimbali zinazowakutanisha  hapa, na  wakati  huu mkiendelea na mkutano wenu, kuna mkutano  unaoendelea kuhusu maandalizi ya malengo mapya ya maendeleo.

Itakuwa vema na ni matumaini yangu  kuwa mtaitumia fursa hii kuwasiliana na  kubadilishana  mawazo na wajumbe wenzenu wanaohudhuria mkutano huo. Lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba  malengo hayo mapya ya maendeleo endelevu utekelezaji wake  unaungwa mkono na Takwimu rasmi na endelevu” akasisitiza.
 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya nchi 30 ambazo ziliteuliwa kushiriki katika majadiliano ya  Kikosi Kazi kuhusu maandalizi hayo ya SGDs   baada ya 2015.

Katika  mzunguko huu wa tisa wa majadiliano   wa hayo kuhusu  SDGs,   Tanzania inawakilishwa na  Dkt. Lorah Madete,  Afisa Mkuu na  mchambuzi wa   Sera kutoka Ofisi ya Rais, Kamisheni ya Mipango.

This entry was posted in

Leave a Reply