Google PlusRSS FeedEmail

MKUTANO WA BARAZA LA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI, DODOMA.

Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Benno Malisa, akifafanua jambo katika kikao hicho.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Martin Shigela, akielezea jambo juu ya mapendekezo ya Kamati ya maboresho. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Maboresho na Uimarishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Hussein Bashe akiwasilisha Taarifa ya Mapendekezo ya kamati yake.

Ndugu Ridhwan J. Kikwete akichangia jambo juu ya taarifa ya mapendekezo ya kamati ya Uboreshaji wa Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM)

Naibu Katibu Mkuu (bara) wa  Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) akifafanua jambo katika kikao hicho cha kujadili maboresho ya umoja huo.

Wajumbe wakifuatilia taarifa ya kamati kwa umakini.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) na mjumbe wa Baraza la vijana Taifa, Ndugu Violet Mzindakaya akiwasha "moto" ndani ya Baraza

Kamanda wa vijana mstaafu, Mzee Kingunge akisisitiza jambo katika kikao hicho.

Wajumbe wa Baraza la Vijana wa Chama Cha mapinduzi wakifuatilia mchango wa mmojawao katika kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Chama,Dodoma.
Wajumbe wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Deus akiwa pamoja na Ndugu Violet Mzindakaya katika kikao cha Baraza hilo.



Baraza la Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa waendelea na vikao ambavyo vinafanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dodoma.

Vikao hivyo ambavyo vilianza rasmi tarehe moja June 1, 2012. Vinaendelea leo hii hapa Dodoma, ambapo hoja mbalimbali zimekuwa zikijadiliwa kwa kina, ambapo vikao vilivyotangulia vimejadili juu ya hoja ya Katiba Mpya na suala la Muungano wa Serikali ya Jamhuri ya Muun gano wa Tanzania. Ambapo wajumbe walichangia hoja mbalimbali za msingi kwa kuzingatia hali ya sasa ya siasa nchini na matukio sambamba na hoja hiyo, kama vile mijadala ndani ya majukwaa mbalimbali juu ya muundo wa Katiba ya sasa, mapungufu yake na mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya na pia mijadala juu ya maboresho ya Muungano.

Pamoja na hayo, kikao kinachoendelea hivi leo,kitajadili juu ya mapendekezo ya jinsi ya kuimarisha na  kuboresho Umoja huo wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mapendekezo hayo juu ya jinsi ya kuboresho umoja huo yametolewa na Kamati maalum ambayo ilipewa jukumu la kupendekeza namna ya kuiboresha UVCCM katika kikao cha Baraza hili kilichokaliwa mnamo tarehe 19/03/2011, ili iweze kukidhi mahitaji ya Siasa za ushindani wa sasa na baadae.

This entry was posted in

3 Responses so far.

  1. KIYUNGI says:

    Bila ccm madhubuti nchi itayumba

  2. Kweli chama kimeshika hatamu, na kinaonyesha jinsi kilivyo iva kisiasa kwa kuwaandaa vijana ipasavyo iliwawe viongozi bora baadae. Lakini cha kusikitisha ni kwambwa tukiwa kwenye wakati ule ambao Wazanzibari wanaulizia nikiasi gani wanashirikishwa kwenye masuala ya utendaji Kitaifa aidha bwana mpiga picha za kikao cha vijana au ndivyo hali ilivyo kwenye kikao chenyewe, hakuna hata mjumbe mmoja wa Zanzibar ameonyeshwa hapo juu au ndio UVCCM hauna wajumbe au viongozi kutoka Zanzibar? Hali hii na nyengine kama hizi zinatupa wakati mgumu sana hata sisi wapenda Muungano wetu kusimama na kuutetea wakati sisi wenyewe ndio tuko mstari wa mbele kupalilia mapungufu. Wazo hili nimelitoa kwa kutafakari manifesto ya CCM ya kudumisha na kuulinda Muungano. Zidumu fikra za wana mapinduzi na wale wote wanaopenda ukombozi wa Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

  3. Jee ndio kweli CCM na hata huu UVCCM hauna hata mzenji mmoja ? Kuanzia viongozi wa juu wa UVCCM hadi wajumbe wa hichi kikao? Au ilitumika Camera binafsi hivyo hizo picha ni za kuonyesha washkaji tu? Kama ni hivyo basi mhariri wa hii blogg ya chama lazima uwe makini zaidi ukizingatia yale yaliyotokea Zanzibar hivi karibuni tusiwape mafuta ya petrol wale wanaotaka kutugawa. Lakini naomba radhi kama mawazo yangu sio sahihi kwani nilijua hiki kikao cha UVCCM ni cha Taifa ( Tanzania na sio Tanganyika) Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu......

Leave a Reply