Google PlusRSS FeedEmail

NAPE AKAGUA CHUO CHA CCM, IHEMI MKOANI IRINGA LEO JUNE 15, 2012

Nape akiwa kwenye banda la mamalishe lililopo njiapanda ya Chuo cha Ihemi na Barabara kuu mkoani Iringa, ambapo alizungumza na mamalishe huyo (kulia) kuhusu changamoto zinazomkuta katika biashara zake.

Msimamizi wa shughuli za ufufuaji Chuo Cha Chama Ihema mkoani Iringa, Simon Nchimba (wa nne kulia) na Nape ( watano kulia) wakitazama eneo la chuo hicho.

Msimamizi wa Chuo Cha Ihemi Simon Nchimba (kulia) akimuonyesha Nape kisima cha maji kilichopo chuoni hapo chenye urefu wa futi saba.

Nape akikagua mashine ya kukata ubao, katika chuo cha Ihemi, mkoani Iringa. Wapili kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emmanuel Mteming'ombe na maofisa wengine wa Chama.

Nape akikagua vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na wanachuo kwa mafunzo ya useremala, chuo cha Ihemi hapo.

  Msimamizi wa Chuo cha Ihemi mkoani Iringa, Simon Nchimba akimpa maelezo Nape kuhusu maenedeleo na changamoto zinazokabili ufufuaji wa chuo hicho. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Deo Sanga 'Jah People'.

Nape na Simon Nchimba wakiwa kwenye moja ya vitanda vilivyoko kwenye mabweni ya chuo cha Ihemi.

Nape akimpa bendera ya CCM, mwananchi aliyeng'ang'ania kupewa bendera hiyo, msafara wa Nape ulipopita eneo la njia panda ya Chuo cha Ihemi.

This entry was posted in

Leave a Reply