SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA MLIPUKO WA BOMU JIJINI ARUSHA
Ni imani yetu kwamba uchunguzi kamili wa mashambulio haya utakamilika haraka na wahusika watakamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria. Tanzania ni nchi yenye hazina ya amani ya muda mrefu. Vitendo vya kigaidi vya aina hii na ambavyo vina mlengo wa kutugawanya kamwe havitavumiliwa na vikomeshwe ili kuondoa wimbi la vurugu zinazoweza kusababisha uvunjikaji wa amani. Tunawasihi Watanzania wote tuwe pamoja na wenye busara na kuondokana na itikadi zozote za kisiasa au ushabiki wa vikundi , aidha na maneno ya kujibizana pasipo sababu.
Ili kuondoa ama kutoamsha hisia za chuki zisizo na manufaa kwa yeyote yule na Taifa kwa ujumla , ni vyema wakati wa majanga kama haya kuachia vyombo vya usalama kufanya kazi yake ya uchunguzi bila kuingiliwa na vyama au kundi lolote kwa maslahi binafsi au umaarufu wa kisiasa . Tunawasihi WaTanzania tuienzi amani yetu iliyolelewa kwa kipindi kirefu na Waasisi wa Taifa letu wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Amani ambayo ni mfano na hadaa kwa wapenda amani kote ulimwenguni.
Imetolewa na idara ya Itikadi Siasa na Uenezi CCM UINGEREZA – UK.
MERGEFORMATINET TAWI LA UINGEREZA – UNITED KINGDOM Website ccmuk.org, Blog ccmuk.org/blog, Facebook page chama cha mapinduzi uingereza, twitter CCMUK 1 Contacts Phone +44 74 04 863333, E-mail – itikadi-uenezi@ccmuk.org