CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga kimefanikiwa kupata wanachama wapya 21,304 ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita na kufikisha idadi ya wanachama 41,425 ikilinganishwa na 20,131 waliokuwepo mwaka 2007.
Katibu wa wilaya hiyo, Khadija Kusaga ameiambia CCM Blog leo kwa simu, kwamba mbali ya wanachama hao pia jumuiya za UVCCM, UWT na Wazazi ziliongeza wanachama wake na kufikia 25,491.
Kusaga alisema kitendo cha watu wengi kuamua kujiunga na CCM pamoja na Jumuiya zake kinaashiria kuimarika kwa chama hicho katika wilaya hiyo ambapo kwa upande wa jumuiya UWT ndiyo iliyoingiza wanachama wengi zaidi ambao ni 11,475 ikilinganishwa na 5,465 waliokuwepo mwaka 2007.
Alisema jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) ndiyo iliyofuatia kwa kuingiza wanachama wengi wakiwa ni 10,507 ambapo kwa mwaka 2007 ilikuwa na wanachama 7,177 huku jumuiya ya wazazi ikifanikiwa kupata wanachama 3,509.
Kuhusu uhai wa chama, Kusaga alisema hadi mwishoni mwa mwaka 2012 wanachama 28,083 walikuwa wamelipia ada zao kwa wakati sawa na asilimia 68 ya wanachama wote ambapo asilimia 32 walikuwa hawajalipa ada kikamilifu.
“Wananchi wameendelea kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi baada ya kuhamasishwa na viongozi wa CCM pamoja na kujionea wenyewe jitihada zinazofanywa na serikali yake katika kuwaondolea kero zao, na kuishi katika hali ya usalama na amani,” alisema Kusaga.
Alisema katika mwaka 2013 chama wilayani humo kimejipanga ili kuhakikisha watendaji wa serikali wanatekeleza kikamilifu ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kutatua kero na adha zinazolalamikiwa na wananchi juu ya maonevu wanayofanyiwa na baadhi ya wafanyakazi wa serikali na taasisi zake. Makatibu wa wenye taarifa za Chama kama hizi watutumie kwa email: nkoromo@gmail.com au ccmmawasilianonaumma@gmail.com au tupigie simu: 0712 498008
hebu waambieni uvccm kuwa mapambano ya vijana yameamia kwenye social network. uvccm jitahidini jamani, mi nashangaa kila nikitembelea uvccm blog mi sioni updated yaani post ya mwisho ni mwaka 2012 kweli jamani tutafika kweli. bado hatujachelewa mi naanza kwa mapambano ya mitandaoni.
hebu waambieni uvccm kuwa mapambano ya vijana yameamia kwenye social network. uvccm jitahidini jamani, mi nashangaa kila nikitembelea uvccm blog mi sioni updated yaani post ya mwisho ni mwaka 2012 kweli jamani tutafika kweli. bado hatujachelewa mi naanza kwa mapambano ya mitandaoni.