Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na wanachama wa CCM kata ya Elerai mara tu baada ya kuwasili kwenye kata hiyo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akibadilishana jambo na mmoja wa wanachama wakongwe wa kata ya Elerai kabla ya kuanza kwa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa Udiwani ya kata hiyo.Mbunge wa Vijana mkoani Arusha , Ndugu Catherine Magige akihutubia wakazi wa kata ya Elerai na kuwataka wakazi wa kata hiyo kutambua thamani ya kura kwa kuichagua CCM.
Naibu Waziri wa Ardhi, Mhe. Goodluck Olemadeye akihutubia wakazi wa kata ya Elerai na kuwaambia CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi kwa wakati na kila kilichoahidiwa Arusha kitafanyika.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Elerai, Mwl.Emmanuel Laizer,na kuwaambia wana Arusha muda wa kufanya maendeleo ni huu na CCM haina kazi nyingine zaidi ya kuleta maendeleo Arusha.
Mgombea wa kiti cha Udiwani kwa tiketi ya CCM, Mwalimu Emmanuel Laizer akihutubia wakazi wa kata ya Elerai kwenye mkutano wa kufunga kampeni.
Bibi na mjukuu wake wakifuatilia kwa makini yale yanayosemwa na viongozi wa CCM wakati wa kufunga kampeni za udiwani kata ya Elerai.
Mbunge wa Vijana Arusha ,Ndugu Catherine Magige akisikiliza kwa makini sera za mgombea wa udiwani wa kata ya Elerai ,Mwl. Emmanuel Laizer.
Mboya akihutubia wakazi wa kata ya Elerai na kuwaelezea kuwa alipotea sana kuishabikia Chadema na amewasihi wakazi wa kata hiyo kutofanya makosa kama kweli wanataka maendeleo.
Wakazi wa kata ya Elerai ,Arusha mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa NEC Itikdi na Uenezi Nape Nnauye maraa baada ya kufungwa kwa kampeni za uchaguzi wa Diwani, juni 14.2013.