Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua juu na kunyesha Kitabu cha Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kulia) na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, wakiperuzi kitabu cha Katiba mpya, baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo kwenye Viwanja wa Karimjee, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Tume ya Katiba mpya, baada ya uzinduzi huo.
Picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Asha-rose Migiro, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Makamu, ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
tunaelekea pazuri,katiba ni ya watu na watu ndio wakusikilizwa wanataka nini japo km ulivyosema haiwezi kumridhisha kila mtu ila naamini inaweza kuwridhisha walio wengi na hilo ndio muhimu
tunaelekea pazuri,katiba ni ya watu na watu ndio wakusikilizwa wanataka nini japo haiwezi kumridhisha kila mtu ila naamini inaweza kuwridhisha walio wengi na hilo ndio muhimu