ASEMA CCM, WATANZANIA BADO WANAGUSWA NA HARAKATI ZA UKOMBOZI WA PALESTINA
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayseer Khalid, kwenye chakula cha jioni, alichomwandalia mgeni huyo na ujumbe wake, kwenye hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam, jana.CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema bado kinaguswa kwa dhati na harakati za ukombozi wa taifa la Wapaletina licha ya kwamba waasisi wa harakati hizo Baba wa Taifa Julius Nyerere na Yaseer Arafat aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo hawapo duniani.
Kuguswa huko kunatokana na udhati uliojengeka tangu enzi za waasisi hao, ambao ulilenga kuhakikisha siyo Tanzania na Palestina tu, bali waafrika wote wanaishi kwa haki na uhuru wakijitawala kwa mujibu wa haki za binadamu duniani.
Hayo yalisemwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula wakati wa chakula cha jioni, alichokianadaa kwa ajili ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO) Tayseer Khalid na ujumbe wake ambao upo nchini kwa mwaliko wa CCM.
Katika chakula hicho cha jioni ambacho alikiandaa kwenye Hoteli ya Protea Couertyard Jijini Dar es Salaam, Mangula alisema, upendo ambao CCM na Watanzania kwa jumla bado wanao kwa Wapalestina ni mzizi ulioachwa na Mwalimu Nyerere ambao hautafutika kamwe.
Mangula alielezea kusikitishwa kwake na vitendo ambavyo uongozi huo wa PLO ulisema, bado vinaendelea kufanywa na Taifa la Israel kukandamiza haki ikiwemo kukalia ardhi ya Palestina.
"Kwa kweli mimi ni miongonimwa watu wanaoguswa sana na hali mnayopambana nayo huko Palestina. Na bila shaka siyo mimi tu kila mwana-CCM na Mtanzania anayejua chimbuko na mgogoro wenu na Israel anaguswa", alisema Mangula.
Naye Makamu Mwenyekiti wa PLO ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu tendaji ya chama hicho, Khalid alisema, licha ya vitimbi ambavyo vimekuwa vikiendelea kufanywa na Waisrael kuingilia mamlaka ya Wapalestina, lakini wananchi wa taifa hilo chini ya uongozi wa PLO hawatakata tamaa.
Alisema, Israel imekuwa ikiendelea ubabe dhidi ya Palestina kutokana na baadhi ya mataifa makubwa kuwakingia ubavu na kuwapatia misaada mingi ya silaha.
Katika mwendelezo wa ziara hiyo ya siku tatu ambayo inamalizika Ijumaa hii, Makamu Mwenyekiti huyo wa PLO na ujumbe wake wa viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho baada ya kuwasili nchini, juzi walikutana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kuwa na mazungumzo kabla ya kwenda Chuo Cha Diplomasia kwenye kongamano maalum.
Ujumbe huo unatarajiwa kuondoka nchini Ijumaa hii, baada ya kukutana na uongozi wa Jumuia ya Wazazi ya CCM kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mangula akifurahi hapa na apale na wageni kabla ya chakulaMjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama Cha PLO,Jehad Abu Znead (kushoto) akimsalimia Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Khamis Dadi kwenye hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, wakati wa chakula cha jioni ambacho Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula aliuandalia ujumbe wa PLO uliopo nchini, Juni 12, 2013. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Amina Makilagi, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Kiongozi wa zamani wa Makao Makuu ya CCM, Hulda Kibacha.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akimsalimia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama cha PLO, Jehad Abu Znead wakati wa chakula cha jioni alichouandalia ujumbe wa PLO ulipo nchini, kwenye hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC,
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza wakati wa chakula cha jioni alichouandalia ujumbe wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) kwenye Hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, Juni 12, 2013. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya PLO, Jehad Abu Znead na Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Balozi wa Palestina hapa nchini, Dk. Nasri Abujais na Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid.
Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer akizungumza kwenye chakula hicho.
Mkao mzima uliokuwa hivi
Mangula na Tayseer wakiongoza kuchukua chakula
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Tayseer Khalid akimpa zawadi maalum, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mangula kwa ajili ya ujumbe wa PLO uliopo nchini, katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, Juni 12, 2013.
Naam zawadi hii ni nzuri: Mangula akifurahia zawadi hiyo
Balozi wa Palestina hapa nchini, Dk. Nasri Abujais (kulia) akitoa neno la kumshukuru Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula ( wapili kushoto), kwa achakula cha jioni alichouandalia ujumbe wa PLO uliopo nchini, katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, Juni 12, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO