Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma.
Itakumbukwa tarehe 16/06/2013 ilikuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa madiwani kwa baadhi ya kata nchini. Uchaguzi huo umefanyika kwenye kata ishirini na mbili (22) kati ya kata ishirini na sita (26) zilizotangazwa kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wazi.
Matokeo tuliyoyapata toka kwenye maeneo yaliyofanya uchaguzi yanaonyesha kuwa kati ya kata 22 zilizofanya uchaguzi CCM tumeshinda kata 16 sawa na asilimia 72.72% na wenzetu wamechukua kata 6 zilizobaki sawa na asilimia 27.28%.
Tunawashukuru sana kote walikoonyesha imani yao kubwa kwa Chama chetu kwa kutupa dhamana ya kuendelea kuwatumikia. CCM inawaahidi utumishi uliotukuka. Hata wale 27.28% walioamua kuwajaribu wenzetu, tunawatakia kila lakheri, kwani wametumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua wanaodhani watawasaidia kufikia malengo yao ya kimaendeleo. Uchaguzi kwenye kata hizi zote umeisha sasa tuwatumikie wananchi.
Kata nne za jiji la Arusha hazikufanya uchaguzi baada ya kuahirishwa kufuatia tukio la kusikitisha la kulipuka kwa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema mjini Arusha tarehe 15/06/2013.
CCM tunalaani tukio hilo la mlipuko wa bomu na matukio yanayofanana na hayo katika nchi yetu. Tunawapa pole wale wote walioathirika na tukio hilo. Ni vizuri serikali ikalichunguza swala hili kwa kutumia muda mfupi na kuhakikisha waliohusika wanapatikana na kuchukuliwa hatua zinazostahili.
Pamoja na kulaani na kuitaka serikali kukomesha vitendo hivi nchini, ni wakati muafaka kwa vyama vya siasa nchini kujitazama upya kwani kuna kila dalili kuwa tukio hili kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari mhe. Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuwa ni la kupangwa, inawezekana limepangwa na Chadema wenyewe.
Hali ya kisiasa jijini Arusha kuelekea uchaguzi huo ilikuwa wazi kuwa wana Arusha walishaamua kuzirudisha kata hizo nne kwa CCM, hasa baada ya kuchoshwa na maandamano na vurugu za kila siku jijini Arusha. Aidha kauli za kukata tamaa za viongozi wa Chadema na vitendo vyao ni dalili tosha kuwa tukio hili lilipangwa na Chadema wenyewe.
CCM tunaendelea kusisitiza na kulaani juhudi za wenzetu kujaribu kujenga umaarufu wa chama chao juu ya damu za Watanzania. Juhudi hizi zinapaswa kulaaniwa na wazalendo wote ndani na nje ya nchi. Tukumbuke asiyekubali kushindwa, si mshindani. Si busara wala uungwana na ni kinyume na utu kutumia majanga ya kutengeneza kama mtaji wa kisiasa.
Lakini CCM tunalaani pia kitendo cha viongozi wa Chadema kujaribu kutumia baadhi ya misiba na majeruhi wa tukio hili kisiasa na mwisho wa siku kwenda kuwatelekeza hospitali baadhi yao baada ya kuwaahidi kubeba gharama zote za matibabu na mazishi.Tunaipongeza serikali kwa kuingilia kati na kuwasaidia waathirika hawa na kuhakikisha wanapata huduma inayostahili.
CCM inarudia kueleza masikitiko yake kwa waathirika wa tukio hili la kinyama na kikatili lisilostahili kuvumiliwa hata kidogo. Kama Chama tumeguswa sana na tukio hili pamoja na kulilaani, tunawasihi watanzania tushindane na kutofautiana bila kupigana na kuvunja tunu ya nchi yetu ya amani na utulivu. Katika demokrasia ya vyama vingi swala la kuvumiliana ni swala la msingi sana katika kufikia ukomavu wa demokrasia hiyo.
Imetolewa;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi.
17/06/2013
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Ideology and Publicity Secretary
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2013
(633)
-
▼
June
(49)
- UFUNGUZI WA MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP DIALOGUE ...
- JARIDA LA KIMATAIFA LAMFAGILIA MOHAMMED DEWJI KWA ...
- MPAMBANO WA MASUMBWI UBINGWA WA DUNIA
- MWENYEKITI UVCCM TAIFA: SIAFIKI SERIKALI MFUMO WA ...
- MEYA WA JIJI LA KAMPALA HOI BAADA YA KUTUOPIWA BOM...
- DK. ASHA-ROSE MIGIRO AFAGILIWA KWA UMAHIRI WA KISW...
- CCM UK WAGUSWA NA MLIPUKO WA BOMU ARUSHA HIVI KARI...
- BUSH NA MKEWE KUJA NCHINI MWEZI UJAO
- MAZALA AWATAKA WAFANYABIASHARA WA NGAZI ZOTE MKOAN...
- RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA ...
- HOSPITALI: CHADEMA WAZUSHI
- MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA BARANI AF...
- CCM YALAANI TUKIO LA MLIPUKO WA MABOMU ARUSHA
- WAZIRI NCHIMBI AWAJULIA HALI MAJERUHI WA BOMU LA J...
- IGP MWEMA AUNDA TIMU KUCHUNGUZA BOMU LILILOUA NA K...
- NAPE AITEKA DONGO BESH NA BASHNET
- NAPE: PUUZENI VITISHO VYA CHADEMA
- WAZEE WA ELERAI WATOA BARAKA ZA USHINDI KWA CCM
- UWT YAUFANYIA SHEREHE KUBWA UJUMBE WA CHAMA CHA PL...
- KINANA AMFUNGULIA MASHITAKA MAHAKAMA KUU PETER MS...
- KATA YA THEMI WACHOSHWA NA SIASA ZA VURUGU
- MANGULA AUKIRIMU CHAKULA CHA JIONI UJUMBE WA PALES...
- NAPE : PIGENI KURA USALAMA UPO WA KUTOSHA
- MAKAMU MWENYEKITI WA PLO AKUTANA NA KINANA, DAR ES...
- MAKAMU KWENYEKITI CHAMA CHA UKOMBOZI WA PALESTINA ...
- CCM YAONYESHA UKOMAVU
- STARS YAREJEA NYUMBANI KUTOKA MOROCCO
- KAMPENI ZA CCM ZA UDIWANI IFAKARA ZAFANA
- CCM YAZIDI KUJIIMARISHA KISHAPU, YAONGEZA IDADI YA...
- CCM MKOA WA VYUO WAPIGWA MSASA NA JANUARY MAKAMBA ...
- CCM DAR YAKUTANA NA UJUMBE WA CHAMA CHA KIKOMUNIST...
- NAPE : KILA LA KHERI TAIFA STARS
- MWALIKO MAHAFALI YA MAKADA WA VYUO WA CCM DAR ES S...
- UJUMBE WA VIETNAM WAKUTANA NA KINANA, MANGULA DAR
- KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA U...
- UJUMBE WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA VIETNAM WAWASI...
- RAIS KIKWETE AWASILI SINGAPORE KWA ZIARA YA KIKAZI...
- RASIM YA KATIBA MPYA, ILKIYOZINDULIWA NA SERIKALI ...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASIMU YA KATIBA...
- MUONEKANIKO WA JUA LIKIZAMA LEO ZIWA VICTORIA
- NAPE AIZAMISHA CHADEMA SENGEREMA
- NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR VUAI ALI VUAI AM...
- No title
- KINANA AFUNGUA SEMINA YA VIONGOZI WA CCM NGAZI ZA ...
- No title
- KINANA AWASILI MJINI SONGEA ASUBUHI HII, KUHUTUBIA...
- CCM YAIFUNIKA MAKAMBAKO, WANANCHI WAFURIKA MKUTANO...
- TASWIRA MBALIMBALI ZIARA YA KINANA MKOANI NJOMBE
- MABALOZI 449 WA NYUMBA 10 WAKUTANA NA KINANA NJOMBE
-
▼
June
(49)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.