NA SHAABAN MDOE NA LILIAN JOEL,ARUSHA.
UONGOZI wa hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya Selian jijini Arusha umekanusha vikali taarifa zilizotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema John Mnyika kuwa serikali ilipeleka maafisa wa usalama hospitalini hapo kwa lengo la kumdhuru mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari pamoja na majeruhi wa mabomu waliolazwa katika hospitali hiyo na kusema ni uzushi mtupu.
Mnyika alisema kufuatia kitendo hicho mbunge Nassari alipiga kelele (yowe) akiwa katika korido ya wodi namba 14 aliyokua amelazwa ili kuomba msaada baada ya maafisa hao wa usalama waliokua wamevalia mavazi ya kitabibu na kubeba vifaa vya kitabibu kumtundikia drip aliyohisi ilikua na lengo la kumdhuru ambayo aliitoa na kuitupa.
Mnyika alitoa kauli hiyo leo alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya mahakama kuu kanda ya Arusha wakati akisubiri wabunge wanne wa chama chake pamoja na wafuasi wao waliohusika na mkusanyiko usio halali katika viwanja vya Soweto jijini Arusha jana
Kwa mujibu wa Mnyika, kufuatia hali hiyo Nassari aliamua kutoroka usiku wa kuamkia leo na kutokomea pasipojulikana ili kujinusuru maisha yake na kwamba Chadema baada ya kupata taarifa hiyo imeamua kumtafutia mbunge huyo hospitali nyingine itakayomtibu kwa gharama za chama hicho.
Pia Mnyika alisema mbali na tukio hilo pia polisi kwa kushirikiana na madaktari wa hospitali hiyo wamekuwa wakiwaruhusu majeruhi wa tukio la mlipuko wa bomu kwenda majumbani kwao kabla ya kupata naafuu ikiwa ni hatua ya kupoteza ushahidi wa tukio hilo.
“Nassari amelazimika kutoroka hospitalini pale jana usiku baada ya kutundikiwa drip na watu tunaowajua ni maafisa usalama iliyokua na lengo la kummaliza ambayo aliitoa na kasha kuanza kupiga yowe katika korido ili kuomba msaada na alifanikiwa kutoroka sasa tutmtibu sisi wenyewe”alisema Mnyika.
Mnyika aliwataja maofisa usalama hao kuwa John Ngowi na Flugence Mark ambao wamekuwepo hospitalini hapo kwa siku kadhaa wakitoa huduma kwa majeruhi wa ajali ya mlipuko wa bomu lililosababisha vifo vya watu nne na kujeruhi zaidi ya 70.
Akijibu tuhuma hizo Kaimu mganga Mkuu wa hospitali hiyo Paul Kisanga alisema si kweli kwamba mbunge huyo alitoroka hospitalini hapo bali alipewa ruhusa katika hali ya kawaida baada ya kuonekana hana tatizo lolote linalomsumbua tangu kufika hospitalini hapo.
Dk.Kisanga alisema mbunge huyo alipewa ruhusa hiyo siku ya Jumanne majira ya saa 9.30 alasiri bila kuwa na malalamiko yoyote kuhusu kutaka kudhuriwa na madaktari anaowadai kuwa ni maafisa usalama waliotumwa na serikali.
Aidha alisema mbunge huyo katika kuondoka kwake hakua na masharti yoyote kuwa anahitaji kupata uhamisho wa kwenda katika hospitali nyingine yoyote kwa matibabu zaidi kwakua hata alipotembelewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alimweleza wazi kuwa afya yake imeimarika.
“mimi namshangaa Nassari kama kweli ametoa tuhuma hizo sisi tumemruhusu baada ya kusema kuwa anaona afya yake imeimarika na hata mbele ya waziri mkuu aliyasema hayo na kwanini hakuyasema hayo kwa uongozi wa hospitali kabla huu ni uzushi”alisema Dk.Kisanga.
Wakati huo huo, Kaimu mganga huyo alisema mototo Fahali Jamali(7)aliyekua melazwa katika chumba cha ungalizi maalumu(ICU)tangu siku ya tukio amefariki dunia jana saa saba mchana kufutia hali yake kuwa mbaya zaidi.
Dk.Kisanga alisema marehemu Fahali alifariki dunia kufuatia majeraha makubwa kichwani yaliyosababisha matundu matatu aliyoyapata kutokana na kulipukiwa na bomu siku ya tukio hilo.
Aidha aliongeza kuwa mara baada ya marehemu huyo kufariki mwili wake ulichukuliwa na jeshi la polisi pamoja na mzazi wake hadi katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru kwaajili ya uchunguzi zaidi kabla ya taratibu za maziko kufanyika.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2013
(633)
-
▼
June
(49)
- UFUNGUZI WA MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP DIALOGUE ...
- JARIDA LA KIMATAIFA LAMFAGILIA MOHAMMED DEWJI KWA ...
- MPAMBANO WA MASUMBWI UBINGWA WA DUNIA
- MWENYEKITI UVCCM TAIFA: SIAFIKI SERIKALI MFUMO WA ...
- MEYA WA JIJI LA KAMPALA HOI BAADA YA KUTUOPIWA BOM...
- DK. ASHA-ROSE MIGIRO AFAGILIWA KWA UMAHIRI WA KISW...
- CCM UK WAGUSWA NA MLIPUKO WA BOMU ARUSHA HIVI KARI...
- BUSH NA MKEWE KUJA NCHINI MWEZI UJAO
- MAZALA AWATAKA WAFANYABIASHARA WA NGAZI ZOTE MKOAN...
- RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA ...
- HOSPITALI: CHADEMA WAZUSHI
- MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA BARANI AF...
- CCM YALAANI TUKIO LA MLIPUKO WA MABOMU ARUSHA
- WAZIRI NCHIMBI AWAJULIA HALI MAJERUHI WA BOMU LA J...
- IGP MWEMA AUNDA TIMU KUCHUNGUZA BOMU LILILOUA NA K...
- NAPE AITEKA DONGO BESH NA BASHNET
- NAPE: PUUZENI VITISHO VYA CHADEMA
- WAZEE WA ELERAI WATOA BARAKA ZA USHINDI KWA CCM
- UWT YAUFANYIA SHEREHE KUBWA UJUMBE WA CHAMA CHA PL...
- KINANA AMFUNGULIA MASHITAKA MAHAKAMA KUU PETER MS...
- KATA YA THEMI WACHOSHWA NA SIASA ZA VURUGU
- MANGULA AUKIRIMU CHAKULA CHA JIONI UJUMBE WA PALES...
- NAPE : PIGENI KURA USALAMA UPO WA KUTOSHA
- MAKAMU MWENYEKITI WA PLO AKUTANA NA KINANA, DAR ES...
- MAKAMU KWENYEKITI CHAMA CHA UKOMBOZI WA PALESTINA ...
- CCM YAONYESHA UKOMAVU
- STARS YAREJEA NYUMBANI KUTOKA MOROCCO
- KAMPENI ZA CCM ZA UDIWANI IFAKARA ZAFANA
- CCM YAZIDI KUJIIMARISHA KISHAPU, YAONGEZA IDADI YA...
- CCM MKOA WA VYUO WAPIGWA MSASA NA JANUARY MAKAMBA ...
- CCM DAR YAKUTANA NA UJUMBE WA CHAMA CHA KIKOMUNIST...
- NAPE : KILA LA KHERI TAIFA STARS
- MWALIKO MAHAFALI YA MAKADA WA VYUO WA CCM DAR ES S...
- UJUMBE WA VIETNAM WAKUTANA NA KINANA, MANGULA DAR
- KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA U...
- UJUMBE WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA VIETNAM WAWASI...
- RAIS KIKWETE AWASILI SINGAPORE KWA ZIARA YA KIKAZI...
- RASIM YA KATIBA MPYA, ILKIYOZINDULIWA NA SERIKALI ...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASIMU YA KATIBA...
- MUONEKANIKO WA JUA LIKIZAMA LEO ZIWA VICTORIA
- NAPE AIZAMISHA CHADEMA SENGEREMA
- NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR VUAI ALI VUAI AM...
- No title
- KINANA AFUNGUA SEMINA YA VIONGOZI WA CCM NGAZI ZA ...
- No title
- KINANA AWASILI MJINI SONGEA ASUBUHI HII, KUHUTUBIA...
- CCM YAIFUNIKA MAKAMBAKO, WANANCHI WAFURIKA MKUTANO...
- TASWIRA MBALIMBALI ZIARA YA KINANA MKOANI NJOMBE
- MABALOZI 449 WA NYUMBA 10 WAKUTANA NA KINANA NJOMBE
-
▼
June
(49)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.