Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akifungua mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW) Mkutano huu wa wiki mbili unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, na unawakutanisha wanawake wa kada mbalimbali kutoka Serikali Kuu na Asasa za Kiraia. Akifungua mkutano, Katibu Mkuu, pamoja na mambo mengine amewataka wanawake kuendelea kutetea fursa za kijinsia, kupinga ubaguzi wa aina zote na kuhakikisha kwamba sauti ya wanawake na watoto wa kike inaendele kusikika katika ajenda mpya za maendeleo baada ya 2015. Kulia kwake ni Muwakilishi wa Kudumu wa Ufilipino katika Umoja wa Mataifa, Balozi Libran Cabactulan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano .
Na Mwandishi Maalum, NEW YORK
Ikiwa imebakia miezi michache kufikia kilele cha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millennia ( MDGs), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amewataka wanawake kuendelea kupigania haki zao pamoja na za mtoto wa kike.
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, ametoa wito huo siku ya jumatatu, mbele ya mamia ya wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kote ambao wapo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW).
Tanzania inawakilishwa katika mkutano huu ambao ni wa wiki mbili na wajumbe kutoka pande zote za Muungano – Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
“Mnajukumu kubwa mbele yenu” akasema Katibu Mkuu. Na kuongeza, imebakia miezi michache kufikia hitimisho la MDGs, na katika kipindi hiki lazima pia tubainishe ajenda za maendeleo baada ya 2015. Ninategemea sana busara zenu na kujituma kwenu katika kuwasilisha kwenye meza, sauti za wanawake na watoto wa kike”.
Ban Ki Moon, amewaeleza wanawake hao kutoka makundi mbalimbali ya jamii kuanzia Serikalini hadi Asasai za kiraia kuwa, alikuwa pia anawategemea katika kupigania na kutetea haki za binadamu kwa wote.
“Hatutawezi kufika mahali pakuwa na dunia yenye hadhi kwa wote mpaka pale tutakapotokomeza tofauti zote za kijinsia. Nipo pamoja nanyi” akabainisha Katibu Mkuu huku akisisitiza kwamba usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake ni moja ya vipaumbele vyake.
Ajenda kuu itakayojadiliwa katika mkutano huu wa 58 wa CSW ni mafanikio na changamoto za utekelezaji wa MDGs. Pamoja na ajenda washiriki wa mkutano huu pia watakuwa na mikutano ya pembezoni yenye maudhui tofauti lakini yote ikilenga katika utekelezaji wa MDGs.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Katibu Mkuu alianisha baadhi ya mafanikio ya utekelezaji wa MDGs, kama vile ongezeko la watoto wanaokwenda shule hasa wa kike, kupungua kwa vifo vya watoto wachanga muda mfupi baada ya kuzaliwa na kupugua kwa pengo la ajira kati ya wanawake na wanaume.
Hata hivyo akasema, katika eneo la ajira, bado wanawake ni wahanga wa malipo duni, mazingira magumu ya kazi, huku wakikosa fursa ya pensheni, bima ya afya na sheria za kazi zinazowalinda.

“Tumetoka mbali, lakini bado tunasafari ndefu tunahitaji vitendo zaidi na sera zinazowajengea uwezo Zaidi wanawake, tunahitaji kuwaona wanawake wengi zaidi serikalini. Nafasi za wanawake katika mabunge zimeongezeka katika mataifa mbalimbali ingawa bado kuna tofauti kubwa za uwakilishi katika ngazi zote” akasisitiza.
Eneo ambalo amelitaja kuwa bado halijatekelezwa vizuri ni eneo la usafi. Akasema kila mwaka watoto 800.000 chini ya miaka mitano hupoteza maisha kwa ugonjwa wa kuharisha. Zaidi ya watu 2.5 bilioni wanakosa huduma sahihi za usafi.
Kama hiyo haitoshi zaidi ya watu bilioni moja wanajisaidia matika maeneo ya wazi. “ tukiongeza utoaji wa huduma za usafi , na kuacha kujisaidia maeneo ya wazi. Hapana shaka tutapunguza sana magonjwa na uchafuzi wa mazingira na kuboresha zaidi usalama wa wanawake na watoto wa kike ambao mara nyingi wamo katika hatari kubakwa kwa sababu tu ya ukosefu wa vyoo safi na salama”.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu, unawahusisha washiriki kutoka pande zote za Muungano, Tanzania Bara na Visiwani. Pichani ni Bi. Asha Ali Abdulla, Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Maendeleo ya Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Tuvako Manongi, Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Jaji Imani Daud Aboud kutoka Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, na Bi. Joyce Mlowe, kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
Baadhi ya Ujumbe wa Tanzania kutoka kulia Bi. Halima Abdulrahman Omar, Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia, Wizara ya Uwezeshaji, Maendeleo ya Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto- Zanzibar, Bi Mhaza Gharib Juma, Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti, Wizara ya Uwezeshaji, Maendeleo ya Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto- Zanzibar, na Bi. Ellen Maduhu, Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu anayeshughulikia Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayohusika na Masuala ya Maendeleo ya Jamii na Haki za Binadamu