MPIGAPICHA WA MAGAZETI YA CHAMA BASHIR NKOROMO APATA TUZO YA UPIGAPICHA BORA TANZANIA
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Pili Mtambalike akimkabidhi zawadi ya king'amuzi cha DSTv na cheti kwa mshindi wa pili katika tuzo ya Mpigapicha Bora Tanzania, Bashir Nkoromo, Mpigapicha huyo alipoenda kuchukua zawadi za ushindi wake, kwenye ofisi za MCT Mwenge, Dar es Salaam, leo. Nkoromo aliibuka mshindi wa pili wakati MCT ilipokuwa ikitangza washindi wa tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT), Machi 14, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Program mwandamizi wa Ubora na Viwango-MCT Alakok Mayombo. (Picha na Saidi Hassan).