- Kampeni zinaendelea vizuri, ingawa kuna malalamiko kidogo juu ya uvunjwaji ama ukiukwaji wa sheria za uchaguzi na malalamiko hayo yapo kwenye vyombo husika yanafanyiwa kazi.
- Malalamiko hayo yanahusishwa na kupigwa kwa Viongozi na kujeruhiwa, wafuasi wa vyama vingine kwenda kufanya kampeni kwenye mikutano ya vyama vingine,kushushwa kwa bendera pamoja na rushwa hasa za kununua shahada za kupigia kura
- Msajiri pia amelaani vitendo vya lugha za kashfa na dhihaka zinazoendelea na kuwaasa wakazi wa Chalinze kuepuka vitendo vya rushwa
- Vyama vya Siasa vimeonywa kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa vyombo husika kila wanapoona inafaa.
- Ni vyama vitano tu vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Chalinze kati ya 21 vyenye usajili wakudumu
Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini maelezo ya Ndugu Sisty Nyahoza Msajili Msaidizi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakati wa mkutano na waandishi hao.