Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na mjumbe wa Kamati kuu ya Chama chama Mapinduzi (CCM) Bw. Jerry Silaa kulia akiteta jambo na Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Bw. Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha ibumila kata ya Mgama halamashauri ya wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa, Jerry Silaa amewaomba wana Ibumila kumchagua Godfrey Mgimwa ili kukamilisha mipango mbalimbali aliyoiacha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Marehemu Dk. William Mgimwa.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na mjumbe wa Kamati kuu ya Chama chama Mapinduzi (CCM) Bw. Jerry Silaa akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Ibumila kata ya Mgama leo
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na mjumbe wa Kamati kuu ya Chama chama Mapinduzi (CCM) Bw. Jerry Silaa wa pili kutoka kushoto akiwa katika mkutano huo kushoto ni mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa na kutoka kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Simiyu,Njalu Silanga, Anthony Mavunde kutoka UVCCM Dodoma, Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassani Mtenga
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na mjumbe wa Kamati kuu ya Chama chama Mapinduzi (CCM) Bw. Jerry Silaa kushoto akishiriki kuimba nyimbo za kuhamasisha katika mkutano huo wa kampeni aliofanyika kwenye kijiji cha Ibumila kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Simiyu,Njalu Silanga na Anthony Mavunde kutoka Dodoma wakijumuika pamoja. nanWa
Wananchi wakimlaki mgombea ubunge wa Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa wakati alipowasili katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama.
Wananchi wakimlaki mgombea ubunge wa Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa kwa kumbeba juu juu, wakati alipowasili katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama.
Kada wa chama cha Mapinduzi Bw. Fredrick Mwakalebela akipigia debe mgombea ubunge wa jimbo la Lalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo leo.
Mgombea ubunge wa jimbo la Lalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa akivishwa mgorole na wazee wa kimila kama ishara ya heshima mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo leo.