Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Novatus Makunga (watatu kushoto) akipokea msaada wa mabati yenye thamani ya shilingi Milioni 5 kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya Mega Trade Investiment ya jijini Arusha, Edmund Rrutaraka, kwaajili ya kusaidia waathirika wa kipunga katika Kijiji cha Kwatito. Katikati yao ni Mkurugenzi wa Masoko wa Mega Trade, Gudluck Kway na wafanyakazi wengine.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mega Trade Investiment wakishusha mabati hayo katika gari.
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga akizungumza baada ya kupokea nsaada huo.
Meneja Mauzo wa Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya Mega Trade Investiment ya jijini Arusha, Edmund Rrutaraka na Mkurugenzi wa Masoko wa Mega Trade, Gudluck Kway wakisalimiana na wanakijiji wa Kwatito baada ya kuwakabidhi msaada huo wa mabati.
Wananchi wakiwa na mabati yao baada ya kukabidhiwa.