Google PlusRSS FeedEmail

KADA WA CCM SHINYANGA AFARIKI DUNIA

Na Chibura Makorongo, Shinyanga
CHAMA Cha Mapinduzi (CCMI mkoani Shinyanga kimepata pigo baada ya kuondokewa na mmoja wa makada wake maarufu ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa CCM katika kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga, Paul Zephania (61) aliyefariki dunia jana baada ya kuugua kwa muda mfupi.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja kifo cha kada huyo kimeacha pengo kubwa kwa wana CCM wa wilaya ya Shinyanga na mkoa kwa ujumla kutokana na juhudi zake za uimarishaji wa chama alizokuwa akizifanya wakati wa uhai wake.
 
Mgeja alisema Zephania ameacha pengo kubwa kwa CCM ambalo litachukua mda kuzibika kutokana na shughuli alizokuwa akizifanya ndani ya chama, na kudai kuwa marehemu alikuwa mkalimu, mpole mwenyekujishusha,kujituma na alikuwa tiyali kuachashughuli zake binafsi kwa ajili ya kukitumikia Chama
 
Akiongoza mazishi ya kada huyo kijijini kwake Iselamagazi jana, Mgeja alisema  marehemu Zephania alijiunga na chama cha mapinduzi tangu mwaka 1978 na mwaka 2002 alikuwa katibu  wa tawi  CCM wilayani humo, na mnamo mwaka 2012 alikuwa mwenyekiti wa kata ya Iselamagazi hadi mauti kumfika
 
“Kwa  kweli CCM tumepata pigo kubwa kwa kuondokewa na kiongozi wetu shupavu ambaye amekitumikia Chama kwa mda mrefu sana (36),tangu ajiunge na CCM alikuwa mchapa kazi na haja wahi kulalamikiwa na mtu yeyote na ndio maana mnaona maelfu ya watu Mmekuja kumpumzisha kwenye makazi yake ya milele kwa sababu alikuwa mtu wa watu’’ alisema mgeja
 
Mgeja pia alitoa pole katika familia ya marehemu pamoja na wakazi wa kata hiyo ya Iselamagazi kuwa chama cha mapinduzi CCM kipopamoja  nao katika kuomboleza kifo cha mpendwa wao na kuwa ambia kuwa wasihuzunike sana kwani mwenyezi mungu kampenda zaidi
 
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni mjumbe wa NEC alitumia fursa hiyo kuwaeleza viongozi mbalimbali wa  madehemu ya dini  waliohudhulia mazishi hayo kwamba CCM inatambua mchango wao katika kuielimisha jamii na kuwaomba waendelee kutoa elimu kwa jamii kupitia mahubiri yao ya kila siku na kuliombe taifa liendelee kuwa na amani.
 
Kwa upande wake msemaji wa familia Emiliani Lucas akisoma historia ya marehemu enzi za uhai wake alisema alizaliwa mwaka 1953 katika kijiji cha Mwang’oye wilayani humo, na kwamba marehemu aliugua ugonjwa wa malaria mnamo Machi 14 mwaka huu na kufariki Machi 18 saa 12 jioni.
 
Marehemu ameacha mjane mmoja, watoto kumi na moja, na wajukuu 21, mazishi hayo pia yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na seriikali mkoani Shinyanga wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM wa mkoa.

This entry was posted in

Leave a Reply