Yosefa Cosmas akitumbukiza kura yake kwenye kisanduku kwenye kituo cha kupigia kura cha Mangalale B, wakati wa uchaguzi huo
Josephine Myagile akitafakari kidogo baada ya kutumbukiza kura yake kwenye kisanduku katika kituo cha Kalenga B
Msimamizi wa kituo cha kupigia kura cha Kalenga B, akimtafutia jina, Joseph Mdibule kwa ajili ya kupiga kura kwenye kituo hichoZaveri Alphonce (70) akijikongoja kwenda kupiga kura kwenye kituo cha Kalenga A katika uchaguzi huo
Wazee wenye matatizo maalum wakisubiri kuitwa kupiga kura kwenye kituo cha Mangalale A, jimbo la Kalenga, wakati wa uchaguzi huo
Watu kwenye kituo cha kupigia kura cha Mangalale A, wakati wa uchaguzi huo
Mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa akizungumza na waandishi baada ya kukagua vituo kadhaa vya kupigia kura, wakati wa uchaguzi huo. Picha zote Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog