Google PlusRSS FeedEmail

KINANA ATOA SOMO PEMBA

  • Awataka wananchi kutokubali kuyumbishwa
  • Awaambia wananchi wa Pemba ,Muungano wa serikali mbili ni rahisi kuusimamia na kuzitatua changamoto zake kuliko wa serikali tatu.
  • Asema Viongozi wao wangekuwa wa kweli wangekuwa na makazi ya kudumu na wananchi wao katika kufanikisha maendeleo,badala  yake wamekuwa watu wa kuingia na kutoka hivyo kukosa muda wa kusimamia maendeleo ya wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye viwanja vya mkutano Gombani ya Kale akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (ZNZ) Ndugu Vuai Ali Vuai tayari kwa kuhutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (ZNZ) Vuai Ali Vuai akihutubia wananchi wa Pemba kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia wananchi wa mikoa miwili ya Pemba katika viwanja vya Gombani ya Kale.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba na kuwataka kuwa makini na viongozi wenye kauli mbili mbili kwani hawana nia njema na maendeleo yao zaidi ya kujifikiria wao binafsi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi kwenye viwanja vya mikutano vya Gombani ya Kale,Pemba na kuwaambia wananchi hao kuwa CCM itaenda sambamba na wapotoshaji wa ukweli.
 Wananchi wakionyesha ishara ya muundo wa Serikali mbili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Gombani ya Kale,Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka na Viongozi wengine wa CCM Zanzibar wakionyesha ishara ya muundo wa Serikali mbili za Muungano wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Gombani ya Kale.
 Mabinti wa UVCCM Pemba wakisoma utenzi wa kumkaribisha KatibuMkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  kutoka kushoto ni Fatuma Juma Ramadhani na Halima Juma Haji kwenye viwanja vya Gombani ya Kale.
 Sheikh Hamisi Ali Hamisi akisoma dua kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Gombani ya Kale Pemba ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihutubia umati.
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka akihutubia wakazi wa Pemba na kuwaambia wawe makini na viongozi wanafiki wa kisiasa.
Makamu Mwenyekiti wa UWT Bi. Asha Bakari Makame akihutubia wananchi wa mikoa miwili ya   Pemba na kuwaambia kuwa wananchi wawe makini na viongozi wanaotaka kuvuruga Muungano wetu.

This entry was posted in

Leave a Reply