Google PlusRSS FeedEmail

MWENDELEZO WA PASAKA;MWANAMUZIKI REBECCA MALOPE KUTUMBUIZA APRIL 4 JIJINI MWANZA

MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope anatarajiwa kutua kwenye jiji la Mwanza a.k.a ROCKY CITY  April 4,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Tamasha la Pasaka 2014

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa Nyota huyo wa muziki wa nyimbo za Kiroho,ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha hilo,ameeleza kuwa msanii huyo alipata kura nyingi kutoka kwa mashabiki waliompendekeza kutumbuiza jijini humo.

“Tunashukuru kwamba baada ya mapendekezo ya mashabiki tuliwasiliana na Rebecca ambaye ameonesha uungwana wa hali ya juu na kutukubalia ombi letu. 

“Lakini pamoja na kukubali ana ratiba ya maonesho sehemu nyingine huko kwao, hivyo ametuambia hatatumbuiza katika mikoa yote ambayo tamasha litafanyika mwaka huu, hivyo tutaangalia wapi tumpangie kulingana na ratiba yake. 
 
“Lakini niwahakikishie mashabiki wetu kwamba msanii huyo tutakuwa naye na sasa ni suala la Kamati ya Maandalizi kuona ratiba yake ilivyo na kisha nasi tumuweke kwenye ratiba yetu ili mashabiki wafurahi,” alisema Msama. 

Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).
Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambao tayari wameshathibitisha ni Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro, Rose Muhando na waimbaji wengine ambao inaelezwa watatajwa hapo baadae.

This entry was posted in

Leave a Reply