Google PlusRSS FeedEmail

URUSI NA CHINA ZA KWAMISHA AZIMIO LA KUIPELEKA SYRIA ICC

Na Mwandishi,New York
Siku  chache baada ya   Bw.   Lakhdar Brahimi ,Mjumbe wa Maalum wa Katibu Mkuu na Muungano wa Nchi  za Kiarabu kujiuzulu na usulushi wa mgogo wa Syria.  Wananchi wa Syria wamepata pigo jingine, baada ya  Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, kushindwa kupitisha Azimio  ambalo  lingeipeleka    Syria katika Mahakama ya Kimataifa ya  Makosa ya  Jinai (  ICC).

Baraza Kuu la   Usalama,  lilikutana  siku ya alhamisi ili kupigia kura  rasimu ya  Azimio  hilo lilowasilishwa na  Ufaransa, lakini   likashindwa kupita baada ya  Urusi na Uchina kupiga kura ya  tururfu kupiga azimio hilo.
Wajumbe  kumi na tatu kati ya  15 wanaounda  Baraza hilo,  walipiga kura ya kuunga mkono  rasimu hiyo.

Kama  Azimio hilo lingepita bila ya kupingwa, basi ICC ingepewa  dhamana ya kuchunguza  makosa yote ya jinai na uhalifu wa kivita kuanzia mwaka 2011 ulipoanza mgogoro  wa wenyewe kwa wenyewe  ambapo zaidi  ya watu 100.000 wamepoteza maisha huku mamilioni wakiwa ni wakimbizi.

Katibu Mkuu  Ban ki  Moon katika salamu zake zilizosomwa kwa niaba yake na Naibu  Wake Bw. Jan Eliason, muda mfupi kabla ya kupinga kura, amesema,  Baraza Kuu la Usalama na lile  la haki za Binadamu yanawajibika kumaliza umwagaji damu na kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa wahanga wa machafuko hayo.

 Akaongeza kuwa  wananchi wa Syria wanayo haki ya msingi ya kupata haki.  Umoja wa Mataifa na wananchama wake wanaowajibu wakuilinda haki hiyo. Kwa kuunga mkono mifumo ambayo itawawajibisha wahalifu wa makosa ya kivita. Na kusisitiza kwamba  ni wazi  kuwa hakuna upande wowote kati ya zinazopingana ambao hauna  kosa.

 Akasisitiza kuwa  kama  wajumbe wa Baraza Kuu  la  Usalama wataendelea kuto kukubaliana kuhusu njia  zinazoweza  kuleta uwajibikaji juu ya uhalifu unaoendelea, hadhi ya  chombo hicho muhimu na Umoja wa Mataifa kwa ujumla itaendelea kuathirika.

“ Tunapozungumzia uwajibikaji, lazima tufikirie si tu kwa pande zinazopingana, bali pia ni lazima tuwafikirie na wale ambao wanaendelea kuchochea mgogoro huu na kuendelea kwa madhara yanayotokana na wao kuendelea kutoa silaha kwa  wale wanaotenda uhalifu” akasema Ban ki  Moon.

Akawasihi wajumbe wa Baraza  Kuu la  Usalama, kuweka pembeni tofauti zao na kufanya kazi pamoja ili kuumaliza mgogoro wa Syria pamoja na kutafuta suluhisho la kisiasa.

Kabla ya  kuwasilisha wa Azimio hilo  mbele ya Baraza Kuu la  Usalama,  kulikuwa na taarifa za kidiplomasia kuwa waandaji wa  Azimio hilo walikuwa wakiziomba nchi ambazo si wajumbe wa Baraza Kuu kuunga mkono hali ambayo si  ya kawaida.

This entry was posted in

Leave a Reply