Google PlusRSS FeedEmail

ZIARA YA KINANA ITOBO WILAYANI NZEGA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Itobo katika Jimbo la Bukene na kuwaambia  waimarishe mahusiano na viongozi wao ikiwa pamoja na kuwaamini katika utekelezaji wa shughuli za kila siku.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Itobo kwenye viwanja vya Itobo Sokoni na kuwahakikishia wananchi wa Itobo kuwa CCM inazidi kuimarika kila siku kwa sababu ndio chama pekee kinacho ongelea matatizo ya wananchi na kuja na majibu ya matatizo hayo.
 Mbunge wa Jimbo la Bukene Ndugu Sulemani Zedi akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Itobo Sokoni ambapo aliwaambia wananchi hao miradi ya maji mitano ipo kwenye hatua za mwisho hivyo tatizo la maji litakuwa limepungua kwa kiasi kikubwa.
 Diwani wa Kata ya Itobo Ndugu Amina Shija akihutubia wakazi wa Itobo na kuwaambia CCM Imejipanga vizuri na itaendelea kuwaletea maendeleo wananchi wake.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe wa uzinduzi wa mradi wa kufyatua matofali wa UWT wilaya ya Nzega unaodhaminiwa na mbunge wa viti Maalum mkoa wa Tabora Munde Tambwe
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa juu ya tanki la maji ambalo ni moja kati ya miradi ya maji ya Itobo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo  ya mradi wa maji katika kituo cha Uchama kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya maji Safi na Taka mjini Nzega Ndugu Samuel Duyigi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na mkulima wa mpunga Ndugu Mohamed Kashinde kuangalia namna mkulima huyo anaendesha kilimo chake cha umwagiliaji,Itobo wilayani Nzega mkoa wa Tabora.







This entry was posted in

Leave a Reply