Google PlusRSS FeedEmail

MAELFU WAFURIKA MKUTANO WA CCM VIWANJA VYA KIBANDAMAITI ZANZIBAR JIONI HII

 MSIHADAIWE SERIALI MBILI ZINATOSHA: Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi kwenye Viwanja vya Kibanda Maiti, mjini Zanzibar, Mei 4, 2014. kueleza kwa nini CCM inawataka Watanzania kuingunga mkono kuhusu msimamo wake wa kutaka Tanzania iendelee kuwa katika mfumo wa serikali mbili ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar baada ya mchakato wa Katiba mpya.

Mjane wa Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Sheik Abeid Amani Karume, Mama Fatuma Karume akizungumza kwenye mkutano huo.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshukuru na kumpongeza Mama Fatma Katume kwa hotuba nzuri 'iliyoshiba'
 Ni serikali mbili tu:  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, akionyesha alama inayotumiwa na chama chake kujinasibu kuwa kinahitaji serikali mbili katika katiba mpya, alipohutubia wananchi katika mkutano huo wa Kibanda maiti, Mei 4, 2014 mjini Zanzibar.
 Kada machacahari wa CCM kutoka Zanzibar, Asha Bakari Machano akihutubia mkutano huo wa Kibanda maiti, Mei 4, 2014.
 Kada mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alitema cheche kwenye mkutano huo, wakati akieleza kwa nini CCM inaona kwamba mfumo wa serikali mbili  katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo unafaa.
 Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib akizungumza kwenye mkutano huo
 Mbunge katika Bunge la Katiba, Emmanuel Nchimbi akizungumza na kutoa ufafanuzi kwamba hata baadhi ya viongozi wa upinzani akiwemo Katibu Mkuu wa CUF Maalif Seif Sharif Hamad wanajua hatari ya mfumo wa serikali tatu kwa taifa la Tanzania
 Kada wa CCM, ambaye pia ni Mbunge katika Bunge la Katiba na Ummy Mwalimu akizungumza kwenye mkutano huo
 Wananchi wakishangilia huku wakionyesha kuunga mkono msimamo wa CCM wa kutaka mfumo wa serikali mbili katika katiba mpoya, wakati wa mkutano huo
 Wananchi wakishangilia huku wakionyesha kuunga mkono msimamo wa CCM wa kutaka mfumo wa serikali mbili katika katiba mpoya, wakati wa mkutano huo
 Baadhi ya wananchi wakijificha mvua kwa miavuli wakati wa mkutano huo, huku wengine wakiendelea kusikiliza hotuba za viongozi kwenye mkutano huo bila kuhofia mvua hiyo.
 Vijana akiwa amejinakshi kwa jina la CCM shavuni kwake akiwa kwenye mkutano huo
 Vijana wakionyesha kuunga mkono msimamo wa CCM wa serikali mbili katika katika mpya, wakati wa mkutano huo.
 Karibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM, Unguja, Juma Borafia, wakati wa mkutano huo.
 Kinana akiagana na baadhi ya wananchi wakliohudhuria mkutano huo. pembeni yake ni Mjumbe wa Kamati Kuu na NEC, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi
 Kinana akiagana na Balozi Seif Ali Idd baada ya mkutabo huo
HAYA BAKIENI SALAMA: Kinana akiwaaga wananchi wote kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa Kibanda maiti baada ya mkutano huo. Picha zote na Bashir Nkoromo

This entry was posted in

Leave a Reply