AJALI YA DALADALA YASABABISHA FOLENI MAGOMENI DAR ES SALAAM
Abiria katika daladala lililokuwa linasafiri kutoka Mwenge kwenda Kariakoo, wakiwa wamekwama kuendelea na safari baada ya daladala hiyo, kugongangana na gari ndogo, eneo la Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam, asubuhi hii. Mbali ya kusababisha adha kwa abiria pia tukio hilo lilisababisha foleni kutokana na magari mengine kushindwa kupita.
ereva wa daladala na wa gari dogo wakijaribu kutafuta suluhu kabla ya Polisi wa Usalama Barabarani kufika eneo la tukio.(Picha zote na Bashir Nkoromo)